Prof. Kitila Mkumbo - Achangia Mtaala Mpya wa Elimu

Hapo hapo nikuulize maswali.. Ulaya ni mataifa mangapi au mataifa gani lugha ya kufundishia ni Kiingereza?

Wote hao walitawaliwa na Muingereza lakini kwa nini waliachana na Kiingereza wakafundishia lugha zao?
Kama tusinge tawaliwa na Muingereza unadhani walotutawala wangefundisha kwa Kiingereza?

Kwa.nini Waingereza walitufundishwa kwa Kiingereza badala ya Kiswahili wakati wao walijifunza Kiswahili?

Na unaweza kunipa sababu?
 
Mwisho, nawakumbusha mwaka 2001 ama 2002 sijui kama ilikuwa hapa #Jamiiforums au Jamboforums, walianzisha thread za Kiingereza, zilikosa jabisa wachangiaji.

Na hata leo hii kama unabisha maneno yangu anzisha mada yoyote inayotamba hapa JF kwa Kiingereza, subiri feed back uone ni wangapi watakuwa interested hata kusoma tu.

Nenda Facebook, Instagram anzisha mada ya kiingereza utakuta 90% wanaochangia sii wakazi wa Tanzania. Unaweza chukia kwa nini watu wako hawachangii au hawafuatilii ukurasa wako kumbe tatizo sio wewe bali LUGHA unayotumia kupeleka ujumbe ndio sio sawa..
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…