Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mbunge wa Ubungo akichangia katika bunge la Bajeti leo amesema ongezeko la bei linaloendelea mtaani sio la kawaida. Amesema ongezeko lililopo sio makosa ya serikali hata hivyo ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua za dharura kudhibiti ongezeko hilo
Ameshauri wizara ya fedha kuja na hatua rasmi ili ziwepo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23. Aidha amesema katika tozo zilizopo serikali ikubali kuondoa walau Tsh 300 katika mafuta ili wananchi wapate unafuu na kuhusu miradi inayoendelea serikali inaweza kukopa ili kui-finance miradi hiyo badala ya kutegemea kodi na tozo ambazo zinawaongezea wananchi ugumu wa maisha
“Naweza kushauri tukachukua Sh. 300 mpaka 400, tukaondoa kwa muda mfupi tukitarajia Julai au Agosti, hali itarudi kawaida. Tukifanya hivyo tutampunguzia mwananchi ukali wa maisha. Hizo fedha zinazopungua kwenye miradi ya maendeleo, Serikali yetu inakopesheka, ikope ili miradi ya maendeleo isisimame,” amesema Prof. Mkumbo.