Prof. Kitila Mkumbo, hili la FCC unavunja Sheria

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Nimesikia Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo leo amewaita Tume ya ushindani (FCC), timu ya Simba na wawekezaji ili kuwasuluhisha kwa kile alichoita migogoro na mkwamo wa uwekezaji Simba.

Huku ni kuvunja sheria, Sheria inataka Tume ya ushindani FCC iwe huru na isiingiliwe katika maamuzi yake. Sheria imeweka wazi mtu asiporidhika na maamuzi ya FCC anatakiwa kukata rufaa kwenda baraza la ushindani yaani Fair Competition Tribunal (FCT). Kama pia hautaridhika na maamuzi ya FCT unatakiwa kukata rufaa kwenda Court of Appeals/ mahakama ya rufani.

Sasa huu utaratibu wa mtu asiporidhika na maamuzi ya FCC Waziri anaingilia kati unatoka wapi? Je ni kwa vile ni Simba? Ni makampuni mangapi hayaridhiki na maamuzi ya FCC na haingilii?

Ndugu Kitila Mkumbo nakuhshimu Ila kwa hili umevinja sheria, acheni taasisi zifanye kazi kwa mujibu wa sheria msilete ushabiki kwenye maswala ya kisheria.
 
Mbona unafanya kama nawe unafanya unachokilalamikia, hata wewe kata FUFAA tuuu.
 
Unawazungumzia mabingwa wapya wa kilab bingwa
 
Wanacho fanya FCC si kuikomoa Simba, FCC wanajua wengi wa mashabiki na wanachama ni ma Mbumbumbu na mwanya uo unataka kutumiwa na Bwanyenye MO kupitia pesa za familia yake kuifanya Simba ni moja ya vitegauchumi vyake. Asicho fahamu Waziri bila kufuata taratibu na Sheria za nchi Bwanyenye MO hawezi kuimiliki Simba. Wenye Simba yao walisha toa ushirikiano kwa FCC kupitia mlango wa nyuma ndio maana Bwanyenye amekwama. Kwasasa anatafuta huruma.
 
Unajua unapoongoza mbumbumbu/Mikia/Bodaboda ni raha sana maana hawaelewi kitu Gabacholi anawageuza kama samaki Bwenyenye gani aweke hela ya familia kwenye klabu bila kupata falda na ndio maana akaunti ya klabu haina kitu pesa zote za klabu haziingii simba Mikia wanasema ili mradi tunashinda acha atunyonye Simba mwenye akili ni Kilomoni na Kigwangwala
 
Mikia wanataka kuleta vurugu fcc. Kama hawajafuata sheria watanyooka tu. Kitila kitulize acha sifa una mambo mengi ya kufanya sio haya. Uwekezaji usio na tija wa nini
 
Wadau wanasema eti ccf wana hoji CEO kapatikana vipi ? Kwann klabu inaongozwa na Mo, ?

Kwa style hii hata ndugu zetu upande wa pili wata kwama kwa style iyo iyo maana huko nako shughuli zote zina ratibiwa na kusimamiwa na MSG kuanzia katibu mkuu mpaka wanao sajili wachezaji
 

Mkuu redio salamu kwako. Naona kama una hoja hapa, hebu weka nyama kidogo juu ya yale yaliyopelekwa FCC kwa mlango wa uani ambao wengi wetu hatuyajui.

Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…