Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Ndugu zangu.
Shibe siyo jambo baya, lakini mlevi akishiba hupata nguvu ya kuongea lolote
Shibe siyo jambo baya, lakini mlevi akishiba hupata nguvu ya kuongea lolote
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Kazi ya Serikali si kugawa Fedha bali ni kutengeneza mazingira ya kupata Fedha na ili kupata Fedha inaamanisha Watu wafanye kazi na kazi zinatoka kwenye biashara.
Ameongeza kuwa "Kazi zinatoka wapi? Wengi wataongelea Serikalini au kwenye mashirika ya Umma lakini mimi nasema kazi zinatoka kwenye Biashara. Ni kweli Serikali inaajiri lakini watu kidogo sana katika watu 100 wanaoajiriwa Tanzania kila siku, Serikali inaajiri watu 5 tu, waliobaki wanaajiriwa na sekta binafsi na sekta binafsi maana yake nini ni biashara".
Akizungumza na CloudsTV leo Nov 29, 2023, amesema Serikali inachokiangalia ni kwa kiasi gani imechangamsha Biashara nchini na biashara hizo zimechamka zaidi wakati huu kulinganisha na miaka 20 iliyopita hata kama hazijafikia kiwango kinachotakiwa.
Kwa mujibu wa Kwa mujibu ripoti ya Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini Tanzania (REPOA) ya 2019, takriban vijana 1,000,000 wanahitimu masomo kila mwaka kutoka Taasisi mbalimbali za Elimu nchini huku idadi ya ajira zinazozalishwa kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ni 250,000 pekee.
Idadi hiyo ni sawa na Wastani wa Muhitimu Mmoja kutumia Miaka 5.5 kupata ajira nchini Tanzania