Prof. Kitila Mkumbo: Kazi ya Serikali sio Kugawa Hela, Serikali inaajiri Watu 5 kati ya 100

Ndugu zangu.
Shibe siyo jambo baya, lakini mlevi akishiba hupata nguvu ya kuongea lolote
 
Huwa wanakera wanaposema wahitimu
Sasa kama tuna wahitimu kwanini wanapeleka wafanyakazi wa ndani kusafisha vyoo vyao na kunyanyaswa huko

Kwanini hawasemi tumepeleka wauguzi au engineers?
Hatuna elimu bali kukariri tu
Waliojaaliwa tena vichwa haswa ni wachache sana na hao wanapigwa vita kama yule mama alietangaza Zika wakati ule akatimuliwa na kupata kazi nje

Wapo ila tunataka watengengenezwe wengi kama hao la sivyo wafunge midomo
 
Mpuuzi apuuzwe mwanzoni.
Zile ajira milioni 3 mlisema mtatoa ilikuwa ni milioni 3 kwa watanganyika milioni 300?
 
Kama anajua hivyo wapunguze kodi, tozo, ushuru na ada kwenye biashara sasa.
Waachane pia na V8, badala yake waanze kutumia IST kupunguza matumizi mabaya ya hela.
 
Sawa hilo liko wazi na ingekuwa yema ikaeleweka hivyo lakini mbona mazingira ya kujiajiri kwa Tanzania ni magumu kupitiliza sio rafiki ukisema uanzishe biashara yako utakumbana na urasimu wa hali ya juu na tozo pamoja na kodi kiasi kwamba kama huna ujasiri lazıma ukate tamaa. Hawa wanasiasa hasa mawaziri wamezoea porojo kila wapatapo jukwaa la kupiga porojo zoo kama hapa Kitila anavyoendeleza porojo anaongelea vijana kujiajiri bila kuwa na mazingira rafiki kwa vijana kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…