Prof. Kitila Mkumbo, mwanasiasa msomi ni somo jema kwa wasomi nchini

bhoke chacha

Member
Joined
Oct 24, 2024
Posts
6
Reaction score
6
Prof. KITILA MWANASIASA MSOMI ,SOMO JEMA KWA WASOMI NCHINI.

Profesa Kitila Mkumbo ambae aliwahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati wa masuala ya kisiasa. Alizaliwa Juni 21, 1971 katika Kijiji cha Mgela wilayani Iramba, Singida.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo ana Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, nchini Uingereza, na Shahada ya Uzamili katika Saikolojia ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Prof. Mkumbo pia ana Shahada ya Kwanza katika Sayansi na Elimu (BSc. Ed.) akiwa amesomea kufundisha masomo ya Baiolojia na Kemia.

Profesa Mkumbo hakuwa na bahati ya kulelewa na wazazi, hivyo alisomeshwa kwa misaada ya ndugu na wasamaria wema na kusoma katika Shule ya Msingi Mgela iliyoko wilaya ya Iramba kati ya mwaka 1981-1987 , akajiunga Shule ya Sekondari Mwenge (Singida) na kusoma kidato cha kwanza hadi cha tano mwaka 1988-1991 kisha akajiunga elimu ya Juu Sekondari ya Pugu kati ya mwaka 1992-1994 mchepuo wa PCB (Fizikia, Kemia na Bailojia).

Kutokana na Mazingira ya Uyatima, Mara baada ya kuhitimu kidato cha sita ,Prof Kitila alifanya kazi ya kuvua samaki katika Bwawa la Mtera-Migoli huko Iringa kutokana na hali mbaya ya kiuchumi aliyokuwa nayo . Katika Wakati ambao ulimkatisha tamaa,ni Mzigo wake wa Samaki kukamatwa na Polisi na kuoza na hivyo kuathiri mtaji na mipango yake.

Pamoja na misukosuko yote hiyo ,Baada ya kuliona Tangazo la Wito wa Vijana Wenye Sifa Kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Maombi yake yalipata msukosuko kwani kiwango cha ufaulu wake kililishangaza Jeshi la Polisi na Kumshauri aendelee na Masomo ya Chuo Kikuu kitu ambacho Prof Kitila alikataa na kuwaomba Wampe nafasi ya Kujiunga na Masomo ya Jeshi la Police.

Baadaye alipata nafasi ya kwenda kujiunga na mafunzo ya polisi kwenye Chuo cha Polisi (CCP) Moshi kwa muda wa miezi miwili lakini alikatisha mafunzo baada ya kuchaguliwa kujiunga Chuo Kikuu.

Profesa Mkumbo alihitimu shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1999 akisomea Sayansi ya Elimu na kufanikiwa kupata ufaulu mkubwa wa daraja la kwanza richa ya harakati zake za Kuiongoza DARUSO kama Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dsm.

Kutokana na Ufaulu Mzuri Ulipelekea Chuo Kikuu cha Dsm Kumpa kazi hapo ya kuwa Ofisa Utawala ambayo aliifanya kwa miaka minne (1999 - 2003) na wakati anafanya kazi aliendelea kusoma shahada ya uzamili (M.A) akibobea katika Saikolojia, alihitimu shahada hiyo mwaka 2002.

Mkumbo ni mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri katika shahada ya uzamili na baada ya kufundisha Chuo Kikuu kwa miaka michache na kupata udahili katika Chuo Kikuu cha Southampton kilichoko nchini Uingereza alikotunukiwa shahada ya uzamivu akibobea katika saikolojia mwaka 2008.

Kutokana na umahili wake kwenye harakati na uwezo wake katika Ushawishi na Ujenzi wa hoja, Mwaka 2010 hadi 2012 Wahadhiri wa Chuo kikuu cha DSM Kupitia Umoja wao wa UDASA ,Walimchagua kwa kura zote kuwa Makamu Mwenyekiti wa UDASA (Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na baadae Walimchagua kuwa Mwenyekiti wa Udasa Oktoba 2014 .

Prof Kitila amekuwa mkuu wa Idara ya Elimu ya Saikolojia na masomo ya Mtaala katika UDSM 2009 -2012, Mhadhiri Mwandamizi kuanzia 2011 -2014, Mkuu wa Kitivo cha Elimu Duce na hatimaye Profesa Mshiriki kuanzia Julai 2014.

Profesa Kitila amekwishafanya tafiti zaidi ya 18 na zimechapishwa katika majarida ya kitaaluma ya kimataifa, amekwishaandika vitabu takribani vitatu, ameoa na ana watoto watatu.

PROF KITILA NA SIASA ZA VYAMA VYA SIASA.
Prof alianza siasa kama mwanachama wa CCM, baadaye alijiunga Chadema na kuteuliwa kuwa mshauri muhimu wa chama hicho, pia akiwa mjumbe wa Kamati Kuu. Mwaka 2014 Profesa Kitila alitangaza kukihama chama chake cha zamani na kujiunga na chama kipya, ACT Wazalendo, akiwa na rafiki yake wa siku nyingi, Zitto Kabwe.

Kwa Watu ambao hawajui;Prof Kitila alikutana na Zitto Kabwe Chuo kikuu cha Dsm ambapo Prof alikuwa Rais wa DARUSO na Zitto akiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar .

Tukio lililowakutanisha Wawili hao pale Nkrumah ilikuwa ni Mijadala ya Kisomi iliyokuwa imeandaliwa na DARUSO. Kutokana na uwezo wa ujenzi wa hoja wa Zitto ukumbini,Prof Kitila alilazimika kumtafuta na kumshangaa kwanini anasoma Zanzibar wakati uwezo na akili alizonazo anapaswa Kusoma UDSM ya enzi hizo?

Zitto alimjibu kwamba alipenda iwe hivyo lakini kwa Bahati mbaya hakubahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa UDSM (Mlimani) na akafanikiwa kupata nafasi Zanzibar.

Prof Kitila ikabidi aanzishe mchakato wa kumjazia fomu na kufanikisha ndoto ya Zitto Kabwe kuchaguliwa Kujiunga na Masomo Chuo Kikuu cha Dsm na huo ndiyo ukawa ni Chimbuko la urafiki na udugu wao. Kwa kifupi Prof Kitila ni Mpenzi na Muumini Mkubwa wa kuamini kwenye Uwezo wa kufikiri na Kujenga Hoja.

Hivyo Prof Kitila hata katika chama chake kilicho kuwa kipya cha ACT yeye alikuwa mshauri mkuu. Watu nilioongea nao kutoka ndani ya ACT walisisitiza kuwa Mkumbo alikuwa na mchango mkubwa na ulioonekana na hata anapokuwa katika taasisi yoyote ile.

PROF KITILA NA HARAKATI ZA UBUNGE.

Profesa Kitila hakuwahi kugombea ubunge katika jimbo lolote hapa Tanzania, muda wake mwingi alijikita katika masuala ya kitaaluma na ushauri wa mikakati ya kisiasa. Japokuwa alipokuwa mwanachama hai wa Chadema alifanya harakati nyingi katika jimbo la Iramba (jimbo linaloongozwa na Mwigulu Nchemba wa CCM) na aliwahi kuingia kwenye misukosuko mingi na hata kufunguliwa kesi ya kisiasa kwa sababu ya harakati zake.

Sifa na nguvu ya kwanza ya Profesa Mkumbo ni kuwa msomi mahiri. Pamoja na kuwa wasomi wengi wanapewa madaraka na wanavurunda kama vile hawakwenda shule, bado mataifa yote duniani hayakwepi wala kukimbia dhana ya kuongozwa na watu walioelimika maana kuna wasomi wengi tu ambao ni waadilifu katika kazi zao, mmoja wao ni Profesa Mkumbo.

Wakati Prof Kitila akiendelea na Majukumu yake ya kutoa Mchango kwenye Ustawi wa Demokrasia kwenye Vyama vya Upinzani na Wakati huo ACT huku akijiandaa na Siasa za Bunge kwa kugombea nafasi ya Ubunge wa Afrika Mashariki kupitia Bunge la JMT alikumbana na mizengwe na kugeuza Dsm ili aendelee na kazi yake ya Uhadhiri, kabla hajaingia Darasani Chuo kikuu cha Dsm alikutana na Simu ya Uteuzi wa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Pamoja na minong’ono mingi iliyokuwepo,Prof alikubali Uteuzi uliofanywa na aliyekuwa Mkuu wa nchi Hayati Mh John Magufuli ambae kabla ya hapo alichukia sana kasumba na utamaduni wa Rais anaetokana na CCM Kuwateua Viongozi au Wanachama kutoka vyama vya upinzani lakni hata kabla Jogoo hajawika aliweza kufanya uteuzi huo kwa kumteua mtu mahili,msomi,mjenzi wa hoja na mwanamabadiliko Prof Kitila.Uteuzi uliowashitua wadau wengi.

Aidha;waliokosoa uteuzi na kumshawishi Prof kukataa,walisahau kwamba Mkuu wa nchi ni Mwajiri Mkuu na ndiye Mkuu wa Utumishi wa umma. Hivyo Mkuu wa nchi anayo Madaraka ya kumpangia majukumu mengine ya umma mtumishi wake pale anapo ona inafaa kufanya hivyo.

Prof Kitila alifanya kazi kubwa sana ya kuongoza Wizara ya Maji kwa kuunda mifumo,kubuni vyanzo vya fedha na kuanzisha miradi mipya ya maji na kuendeleza ile ya zamani ili kuweza kuikwamua nchi kutoka kwenye mkwamo mkubwa wa huduma ya Maji na ndiyo Wakati alio Mshauri Rais kuanzisha Wakala wa huduma za maji Vijijini (RUWASA).

Kutokana na utendaji kazi wake mkubwa,CCM iliweza kumwamini na kumpa majukumu mazito ya kukishauri chama na uandaaji wa nyaraka mbalimbali za namna ya kukisuka chama na kukihuisha katika mazingira mapya ya siasa za kizazi kipya.

Ni wakati huo ambao Prof Kitila alianza kujiandaa kugombea Ubunge Jimbo la Ubungo mwaka 2020,alitangaza nia hiyo Kupitia Akaunti yake ya Mtandao wa Twitter kuwa atagombea Uchaguzi Mkuu uliootarajiwa Kufanyika Oktoba Mwaka huo na kufanikiwa kushinda nafasi hiyo ya Ubunge.

UWEZO WA PROF KITILA.

Ukiniuliza, mmoja kati ya wasomi wanaojua majukumu yao na wanayasimamia sana, nitakwambia Profesa Kitila ni mmoja wao. Kwenye eneo hili ile dhana ya CCM kuwa na hazina kubwa ya Viongozi kwenye Succession Plan Wamefuzu.

Lakini jambo la pili, yeye ni mwanademokrasia thabiti na anayependa demokrasia iwe katika vitendo. Msomi huyu ni mmoja wa watu wanaoamini katika kujenga hoja na wanaopenda hoja zishindanishwe na zijadiliwe kwa uwazi na kisha hoja yenye mashiko ndiyo ipitishwe na amekuwa kete muhimu kwa Wakati huu ambao hoja imekuwa ni injini ya uendeshaji wa Siasa za nchi.

Ukitembelea ukurasa wake wa Facebook utaona watu wanaandika jambo lolote na humuoni akigombana nao, anapingwa waziwazi na wakati mwingine anatukanwa lakini anaacha uhuru wa wanaompinga na kumtukana uendelee. (Mimi binafsi nimekuwa sipendi mtu anitukane au anidhalilishe kwenye mitandao, napenda kupingwa kwa hoja na si kutukanwa na nakumbuka kila aliyenitukana niliishia kumuondoa miongoni mwa marafiki).

Jambo la tatu ambalo ni nguvu na sifa ya Profesa Mkumbo ni kubahatika kuwa kiongozi kila alipokaa, kusoma, kufanya kazi n.k. Amebahatika kuwa kiongozi tangu akiwa mdogo, nidhamu na kuwajali wenzake viliwavuta watu waliomzunguka kumtumia yeye awe mwakilishi wao. Amekuwa kiranja tokea akiwa Shule ya Msingi, Sekondari na Sekondari ya Juu. Uwezo huu wa kiuongozi uliendelea hata alipokuwa Chuo Kikuu (UDSM) kwani alichaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso) kati ya mwaka 1998 - 1999.

kwa mfano kumudu kuongoza Daruso na kisha akapata daraja la kwanza katika shahada yake siyo jambo dogo. Mimi nimekuwa kiongozi wa Daruso na sikudhani kama kiongozi wa Daruso anaweza kupata First Class, Uongozi ule ni kushughulikia matatizo ya wanafunzi kila kukicha huku vikao vya menejimenti vya chuo vinavyoamua masuala ya wanafunzi vikiendelea kila kona na unapaswa kuwapo kote huko. Pia kuongoza Udasa, Duce, na timu za kiushauri katika mipango na mikakati ya Chadema , ACT na CCM. Mtu anayemudu majukumu mengi namna hii ndani ya CCM anaweza kuwa Profesa Kitila pekee na huenda baada ya Mh Samia Suluhu Hassan kumaliza term yake hapo itakapofika mwaka 2030 chama hicho kitakuja kuhitaji mgombea urais atakaekuwa na huruka ya Prof Kitila atakayemudu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja .

Prof Kitila yeye ni mmoja wa wataalamu wachache waliobobea na wenye uwezo mkubwa katika eneo la Elimu ya Saikolojia hapa nchini

Prof Kitila ni mtu muhimu kwenye kuendeleza mchango wa ukuzaji wa fikra katika jamii ya Watanzania ambayo ina matatizo makubwa katika kufanya siasa za kuvumiliana na kukubali changamoto mpya.

WAJIBU ALIO NAO SASA WA KUMSAIDIA MH DR SAMIA SULUHU HASSAN KUENDELEA KUONGOZA JMT KUPITIA UCHAGUZI MKUU 2025.

Prof Kitila anapaswa kutumia kipawa alichonacho kukabiliana na Vyama vya Upinzani kwa kutumia takwimu kujibu hoja zitakazoibuliwa na vyama vya Upinzani. Ni wazi kuwa kazi kubwa imefanywa na SSH toka apokee kijiti cha uongozi wa nchi kutoka kwa Hayati JPM. Kazi iliyofanywa na Mh SSH Rais wa JMT inahitaji kutafsiriwa katika lugha rahisi kupitia kwa Wasomi nguli kama Prof Kitila.
 
Subiri waje wabaya wake wasema ana PhD ya Saikolojia, hawezi kuongoza Wizara ya Mipango.

Ni mmoja wa wasomi makini sana.
 
Kwa bahati mbaya sana, hao Wanasiasa wasomi wakiingia huko Chama tawala wanakuwa Kama vile wamerogwa, akili zao zinakuwa hazifanyi kazi sawasawa.
Wanageuka kuwa Kama na akili za Mtu zumbukuku vile!
 
Hawa wasomi wangekuwa na elimu wasingelilia pesa za misaada kutoka ulaya.....huo usomi wao tutakuja kuuthibitisha kipindi hiki ambacho trump amezuia misaada
 
Profesa hakuhama CHADEMA, alifukuzwa kutokana na jaribio la kufanya uasi .
 
Subiri waje wabaya wake wasema ana PhD ya Saikolojia, hawezi kuongoza Wizara ya Mipango.

Ni mmoja wa wasomi makini sana.
Kabisa,ni miongoni mwa Wasomi wachache ambao wamestawi vyema kwenye taaluma zao na kwenye tasnia ya Siasa walistawi vyema.
 
Kwa bahati mbaya sana, hao Wanasiasa wasomi wakiingia huko Chama tawala wanakuwa Kama vile wamerogwa, akili zao zinakuwa hazifanyi kazi sawasawa.
Wanageuka kuwa Kama na akili za Mtu zumbukuku vile!
Siyo Wanasiasa Wote,Na siasa haiwezi ikabaki mikononi mwa kundi la watu ambao hawajasoma. Tuwape Moyo wasomi wachache wanaoingia kwenye nafasi za kisiasa
 
Back
Top Bottom