Prof. Kitila Mkumbo: Pato la kila Mtanzania limeongezeka nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema katika ripoti ya Hali ya Uchumi nchini imeonesha Pato la Wananchi (GDP Per Capital Income) limepanda kutoka Dola za Marekani 399.5 (Tsh. 322,397) mwaka 2000 hadi kufikia Dola 1,200 (Tsh. 2,880,000).

Akifafanua zaidi amesema "Tukisema hivyo watu wanauliza mbona hizo fedha mbona mfukoni sina, hesabu zake ni kukusanya mapato ya Nchi nzima ambayo yakafikia Tsh. Trilioni 141 unagawanya kwa idadi ya Watu ndio unapata pato la kila mtu."


Your browser is not able to display this video.
 
Akifafanua zaidi amesema "Tukisema hivyo watu wanauliza mbona hizo fedha mbona mfukoni sina,
Kwahio anajua kabisa Statement yake inahitaji ufafanuzi
hesabu zake ni kukusanya mapato ya Nchi nzima ambayo yakafikia Tsh. Trilioni 141 unagawanya kwa idadi ya Watu ndio unapata pato la kila mtu"
Kwanini asielezee tu hivyo; kwahio kipato cha kila mtu mtaani kwenu kimeongezeka baada ya tajiri mmoja kuamia kitaa..., Kwanini tu asiseme kipato cha mtaa kimeongezeka LAKINI sio kipato cha kila Mtanzania
Haya mambo ya massaging and interpreting the numbers ni kuleta noise kwa watanzania, wajikite kwenye Sera za kuongeza ujira wa Wabangaizaji wala hawatakuwa na sasabu ya mdomo kujaribu kulidanganya sikio
 
Huyu asitufanye hamnazo
Madaraka yamemlevya sana
Kila siku ni yeye pelepele blablahn&$ko anatuchosha
 
Kweli anatuchosha sana siku hizi amekuwa mjibga mjibga sana na matamko yakee......hayana maana kwa mtanzania....
 
Hivi Wanasiasa huwa wanatuchukuliaje aisee[emoji848]
 
Amepigaje hapo? 🤣🤣
Hili zee linatutafutia dhambi ya kutukana wazee
 
" The main difference between FOOLS and BRAVES is that, BRAVES speak when they have something to say, but FOOLS speak because they have to say something."
 
Hivi huyu mtu anajua athari za upuuzi anapuongea?
 
Huyu asitufanye hamnazo
Madaraka yamemlevya sana
Kila siku ni yeye pelepele blablahn&$ko anatuchosha
Si uchukue hiyo jumla ya makusanyo ya trillion 141 kisha uigawanye kwa idadi ya watanzania wote ili usichoshwe na mtu
 
Hivi huyu mtu anajua athari za upuuzi anapuongea?
hebu msaidizi ndugu mchumi makusanyo ya trillion 141 ukigawanya kwa waTanzania wote inakua kiasi gani.

Maana naona unakasirikia hata hela iliyokusanywa kutoka kwako?🤣
 
hebu msaidizi ndugu mchumi makusanyo ya trillion 141 ukigawanya kwa waTanzania wote inakua kiasi gani.

Maana naona unakasirikia hata hela iliyokusanywa kutoka kwako?🤣
Kwa hiyo nawe umeishia hapo.

Nadharia na facts vinapaswa kuoana na siyo kukimbiana.

Alichoongea ni upumbavu na wewe unashaubikia kwa sababu unanufaika na huo upumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…