Wakurugenzi waajiriwe na Baraza la madiwani..
Kwasasa Sheria inayounda mamlaka ya serikali za Mitaa, inawapa Madiwani mamlaka ya kinidhamu kwa Watumishi wa umma.
Suala hili limekuwa Ni kero sana has katika nchi yet ambayo watu wengi tunaishi kwa Unafiki na CHUKI.
Kutokana na suala hili, mpaka sasa Kuna mapendekezo kuwa badala ya Madiwani kuwa na mamlaka ya kinidhamu kwa Watumishi wa umma, Ni Bora Jambo hili likawa kwenye mamlaka ya Tume ya Utumishi mkoa.
Pili vigezo vya mtu kuwa diwani vipitiwe upya
Vipitiwe upya na Nani?
Wananchi wetu wakoje, maana isije kuwa unaweka vigezo ambavyo sasa itabidi Wananchi waanze kutafuta watu kutoka nje ya maeneo yao kuja kuwa Viongozi kitu ambacho siyo demokrasia.
Demokrasia Ni kuchagua mtu unayempenda na unaridhika naye hata kama Ni hajui kusoma Wala kuandika.
tatu wananchi wapewe nguvu ya kuondoa diwani yeyote bila kusubiria uchaguzi kwa ku sign petition ya kura kadhaa zenu tunaanza mchakato,mshindi wa pili anachukua nafasi bila kuingia kwenye uchaguzi mwingine..
Siasa zinazohusisha watu wengi, Ni rahisi kuwa manipulated.
Tunashiriki VICOBA na SACCOS zinazoongozwa kidemokrasia na tunaliona hili. Siyo Jambo rahisi kuweka msimamo was pamoja kwenye taasisi za watu wengi wenye itikadi, hisia na imani tofauti.
Pili uwakilishi uhusishe vyama vya hiari kama NGOs,makundi maslahi nk.
Kwa sababu uzoefu unaonyesha Baraza la madiwani haliwezi kabisa kuisimamia Halmashauri ndio maana wizi na ujenzi wa miradi chini ya kiwango na inefficiency ni kubwa kweyutoaji huduma achilia mbali maamuzi ya kisenge kisenge yasiyojali maslahi ya umma..
Hii ndio inasababisha Serikali kuu iwe inaonekana iko in charge moja kwa moja.
Na jambo jingine kila Halmashauri ijitegemee.Hii ya kuchukua pesa za Ubungo kupeleka Lindi haikubaliki ,inalea uzembe.
Suala la miradi kuwa chini ya kiwango sidhani kama issue ni Madiwani.
Issue kubwa hapa Ni SIASA ZA MASLAHI.