Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo, amewakaribisha rasmi wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia kuwekeza katika sekta mbalimbali za kimkakati nchini Tanzania.
Prof. Mkumbo amebainisha kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kuisaidia Saudi Arabia kupata usalama wa chakula kupitia uwekezaji kwenye kilimo cha biashara na viwanda vya uchakataji wa mazao. Akifafanua zaidi, alisisitiza kuwa mwelekeo wa sasa wa serikali ni kuuza nje ya nchi bidhaa zilizoongezewa thamani ili kutengeneza ajira kwa wananchi.
Soma pia: Prof. Kitila Mkumbo: Tanzania haitakubali kupangiwa marafiki wala maadui
Katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, Prof. Mkumbo alisema serikali imeweka mkazo mkubwa kwenye sekta ya viwanda vya uzalishaji wa mashine, dawa, na uchakataji wa madini nyeti (critical minerals). Pia, aliwaalika wawekezaji hao kuwekeza kwenye sekta ya nishati mbadala, hususan nishati ya jua (solar), ili kukidhi mahitaji makubwa ya umeme kuelekea mwaka 2030 na 2050.
Akiangazia sekta ya madini, Prof. Mkumbo alitoa msimamo thabiti wa serikali na Mheshimiwa Rais kwa kueleza kuwa enzi za kusafirisha madini ghafi moja kwa moja kutoka ardhini kwenda nje zimepita, na kwamba kwa sasa msisitizo mkuu ni kujenga viwanda vya kuchakata madini hayo hapa hapa nchini.