Prof. Kitila: Pato la Taifa kwa Mtu umeongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia Milioni 3.5

Prof. Kitila: Pato la Taifa kwa Mtu umeongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia Milioni 3.5

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo leo Juni 11, 2026 amesema wastani wa Pato la Taifa kwa Mtu umeongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia shilingi 3,544,124 (dola 1,390) mwaka 2025, ikilinganishwa na shilingi 3,299,637 (dola 1,264) mwaka 2024.

Akiwasilisha Bungeni taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 pamoja na mpango wa maendeleo wa 2026/2027, Prof. Mkumbo amesema maboresho ya takwimu za Pato la Taifa yamefanyika kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ambapo mwaka wa kizio umebadilishwa kutoka 2015 hadi 2019 ili kuakisi hali halisi ya uchumi wa sasa.

"Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio za mwaka 2019, pato halisi la taifa lilikuwa kwa wastani wa asilimia 5.6 mwaka 2025 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.6 mwaka 2024.

Mheshimiwa Spika, kwa bei za mwaka husika, pato la taifa lilifikia shilingi trilioni 234.1104 mwaka 2025, sawa na dola za kimarekani bilioni 91.81 ikilinganishwa na shilingi trilioni 211.975 sawa na dola bilioni 81.2 kwa mwaka 2024. Kutokana na mwenendo huu, wastani wa pato la taifa kwa mtu uliongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia shilingi milioni 3.544,124 sawa na dola za kimarekani 1,390 kwa mwaka 2025, ikilinganishwa na shilingi milioni 3.299,607 sawa na dola 1,284 kwa mwaka 2024."

​
Sekta zilizokuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa 2025
Kilimo kilichangia asilimia 24.3
Ujenzi asilimia 11.9
Uchimbaji wa madini na mawe asilimia 10.3
Biashara na matengenezo asilimia 8.6
Usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.3

Sekta zilizoongoza kwa ukuaji
Fedha na bima asilimia 15.7
Umeme na gesi asilimia 11.8,
Uchimbaji wa madini na mawe asilimia 9.4
Habari na mawasiliano asilimia 8.8
Sanaa na burudani asilimia 8.5
Usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.0
 
NImeishi na Bibi yangu kwa muda mrefu hadi alipotangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu amrehemu, Nyamhalwa Magese huko, alipo.

Katikamakuzi yetu,Bibi alituamini sha kuwa " Mapropesa" ni waongo na matapeli ambao huwalaghai watu mchana kweupe.

Hawa ndio wafanya mazingaombwe na walaghai wa kuuuza nyumba au viwanja visivyo vyao, hawa ndio wakiuuza almasi na dhahabu bandi. Alitufundisha kukaa mbali na nao kwani sio wakweli.

Leo, miongo kadhaa nimeendelea kuyasikia na kuyashuhudia mafundisho ya Bibi , juu ya mapopesa, ni waongo na walaghai.

Huko kwenye hilo jengo linaliitwa bunge wamejaa na aghalabu hutokea nyakati wao wenyewe, wanabaini kuwa hapa " tunapangwa" ndio unasikia wanasema ".... muongo sana"

Sasa huyu hapa mwingine kwamba pato langu ni mil 3.5,kwa kazi ninayolipwa kutwa buku saba!. Asante Bibi upumzike kwa amani.
 
That is an economical theory, not a reality. Unachukua GDP unagawa na population number. Mambo fulani ya kupumbaza akili za watu.
 
Wapo watu wengi wanaishi kwa mlo mmoja tu kwa siku
kazi hakuna vibarua hakuna
 
Kleptocracy system at its best practice.

Ofisi ya takwimu yatakiwa kuwa huru kutoa data bila kuingiliwa na kupangiwa.

Bado kama taifa tuko kwenye safari ndefu.
 
Back
Top Bottom