Prof. Kitila: Rais anapofanya ziara haendi kutafuta MISAADA. Hatutakubali kuchaguliwa rafiki wala adui

Prof. Kitila: Rais anapofanya ziara haendi kutafuta MISAADA. Hatutakubali kuchaguliwa rafiki wala adui

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/27, leo Juni 11, 2026, amempongeza Rais Samia kwa ziara yake nchini Urusi, huku akisitiza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha msimamo wake wa kihistoria wa kutofungamana na upande wowote, uliowekwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Amesema ziara ya Rais Samia nchini Urusi ni sehemu ya mkakati huo wa kutafuta washirika wa maendeleo na si misaada. Kitila ameeleza kuwa Tanzania haiko tayari kuchaguliwa marafiki wala maadui na taifa lolote, bali itaendelea kushirikiana na mataifa yote ya Mashariki na Magharibi kwa misingi ya kuheshimiana, usawa, na kutokuingiliana katika masuala ya ndani.


"Nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake makini. Kwa kipekee namshukuru na kumpongeza kwa ziara yake ya kihistoria na yenye mafanikio makubwa aliyoifanya hivi karibuni katika taifa kubwa la Urusi, akiwa ni Rais wa pili wa Tanzania kufanya ziara rasmi nchini Urusi.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu kuzingatia kuwa ziara ya Mheshimiwa Rais nchini Urusi ni sehemu ya utekelezaji wa falsafa yake ya kuifungua nchi, au kile kinachoitwa pragmatism, ambayo inazingatia uhalisia wa mambo kwa wakati husika katika kufanya maamuzi ya msingi ya kisera, ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Katika falsafa hii, anapofanya ziara za nje, Mheshimiwa Rais anaenda kutafuta washirika—yaani partners wa maendeleo. Haendi kutafuta wafadhili au wadhamini, kwa maana ya sponsors au patrons. Mheshimiwa Rais anaenda nje kutafuta fursa za biashara na uwekezaji, na sio kutafuta misaada.

Mheshimiwa Spika, na katika kusaka fursa za biashara na uwekezaji, hatutachagua wapi pa kwenda, wala hatutakubali... wala hatutakubali kuchaguliwa rafiki wala adui.

Kama alivyowahi kusema Deng Xiaoping, Rais wa zamani wa China:

"It doesn't matter whether a cat is black or white, as long as it catches mice."

Mheshimiwa Spika, msimamo huu wa Rais wetu wa kukataa kuchagua marafiki wala adui sio mgeni kwa nchi yetu. Mara baada ya nchi nyingi za Afrika kupata uhuru miaka ya sitini, lilitokea wimbi na shinikizo kubwa la kuzisukuma nchi za Afrika kuchagua upande wa kushoto au wa kulia, au upande wa Magharibi au wa Mashariki kama ilivyojulikana wakati huo.

Kufuatia shinikizo hilo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza na Baba wa Taifa letu, aliweka msimamo wa wazi ambao ndio msimamo wetu unaotuongoza leo aliposema—naomba nimnukuu:

"We desire friendship with the countries of the East as well as with those of the West, and on the basis of mutual respect and non-interference in internal affairs. We will not allow any of our friendships to be exclusive. We will not allow anyone to choose our friends or our enemies for us."
 
Back
Top Bottom