Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kutunza hali ya usalama na amani nchini tangu alipoapishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mabibo, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, ambapo pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila alisema, "Kazi ya kwanza ya Rais ni kuhakikisha kwamba nchi anayoiongoza ina amani, usalama na utulivu. Rais Samia amefaulu katika hili, ndiyo maana anaitwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
Alisisitiza kwamba Tanzania bado ina amani na utulivu, licha ya changamoto zinazoweza kutokea wakati wa mabadiliko ya uongozi. “Nchi zinapoondokewa na Mkuu wa Nchi huwa zinayumba, lakini Rais Samia amefanikiwa kuibakisha Tanzania kuwa salama,” aliongeza Prof. Kitila.