Prof Kitila: Serikali Imepokea Ushauri wa Kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar

Prof Kitila: Serikali Imepokea Ushauri wa Kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Akichangia mada kwenye kongamano la Uwekezaji kati ya China-Tanzania msomi wa UDSM ameshauri Serikali kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar Kwa kushirikiana na China.

Akijibu hoja hiyo Waziri wa uwekezaji prof.Kitila mkumbo amesema Serikali Imepokea Ushauri na itaufanyia kazi.
---
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali imeyapokea mapendekezo na maoni yaliyotolewa juu ya ujenzi wa daraja kutoka Tanzania bara (Dar es Salaam) kwenda visiwani Zanzibar.

Mbali na hilo amesema matumizi ya pesa ya China (Yuan) na shilingi ya Tanzania katika shughuli za biashara na uwekezaji na nchi ya China, vilevile Serikali imechukua kwenda kuyafanyia kazi kwa kuyachakata.

Mapendekezo hayo yametolewa na Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza kwenye Jukwaa la mashirikiano ya maendeleo kati ya China na Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya diplomasia ya mataifa hayo mawili.

Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 22, 2024, Profesa Moshi amesema China ni rafiki wa kwanza wa Tanzania katika nyanja mbalimbali, hivyo ameomba wawekezaji na Serikali ya nchi hiyo kujenga daraja huku akipendekeza liitwe Daraja la Karume/Nyerere.

Aidha, Profesa Moshi ameomba kuibadilisha reli kati ya Tanzania na Zambia (Tazara) kuwa reli ya kisasa kama zilivyo za China kwa ajili ya kuendana na dunia ya sasa.

"Katika matumizi ya pesa nashauri tutumie Yuan na Shilingi kwa sababu dola ni gharama kubwa, tukitumia pesa za ndani basi tutapunguza hasara na athari mbaya za dola kwenye ulipaji wa deni, mfumuko wa bei na gharama ya maisha," amesema.

Aidha, msomi huyo amesema itakuza matumizi ya sarafu za ndani katika miamala ya kibiashara kama njia ya maendeleo ya kiuchumi.

Sambamba na hilo, Profesa Moshi ameomba uwekezaji katika kilimo cha kisasa ili kuongeza tija, kwa nia ya kuongeza kasi ya kupunguza umaskini, na kukuza uchumi shirikishi zaidi.

Vilevile, amehamasisha matumizi ya vyanzo mbadala vya nishati, yaani jua na upepo, kwa nia ya kupunguza utegemezi wa maji. Pia, kwa upande mwingine ameipongeza nchi ya China kwa kukitangaza Kiswahili.

Katika kuyajibu hayo alipoulizwa na Mwananchi wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya kongamano hilo, Profesa Mkumbo amesema Serikali imeyapokea yote hayo.

"Ni hoja, mawazo na maoni mazuri, tumezipokea tunajua wasomi wamefanyia utafiti mfano kwenye kilimo, daraja na uwekezaji, mimi kama waziri wa mipango na anayesimamia dira ya Taifa tumepokea," amesema.

Sambamba na hilo, amesema uboreshwaji wa reli ya Tazara inayoziunganisha nchi za Tanzania na Zambia huku akisema hadi sasa tayari wameshakubaliana na China kushirikiana namna ya kuifufua reli hiyo.

"Waziri wetu wa uchukuzi ataenda kusaini mkataba na kampuni ya China katika safari ijayo ambapo China imealika nchi 52 za Afrika watasaini kwa ajili ya kuimarisha reli ya Tazara."

Akieleza zaidi, Profesa Mkumbo amesema China kwa sasa inaongoza katika uwekezaji na Tanzania ikiyapiku mataifa ya magharibi na nchi yetu itazidi kuiga China kwakuwa walishawekeza kwenye elimu na uchumi wa viwanda kisha wakaaga umasikini.

"Lazima tuwatoe watu kwenye uchuuzi kwenda kwenye uzalishaji wa viwanda na Serikali inazidi kuweka mkazo kwenye maeneo hayo," amesema Profesa Mkumbo.


My Take
Mfikirie pia kujenga daraja au Trum kati ya Tanzania-DRC Congo via Lake Tanganyika
 
Hivi Kwa hali ya Uchumi wetu tutaweza kweli hizo gharama za Ujenzi?

Labda kama tutajenga Kwa njia ya PPP then tukawa tunatumia Kwa kulipia kama ilivyo daraja la Mwalimu Nyerere - Kigamboni

Ni wazo zuri kulitekeleza kama Kuna hiyo nafasi
 
Hivi Kwa hali ya Uchumi wetu tutaweza kweli hizo gharama za Ujenzi?

Labda kama tutajenga Kwa njia ya PPP then tukawa tunatumia Kwa kulipia kama ilivyo daraja la Mwalimu Nyerere - Kigamboni

Ni wazo zuri kulitekeleza kama Kuna hiyo nafasi
Litajengwa Kwa njia ya PPP yaani linajengwa na private sector so litakuwa la kulipia
 
Utapeli upi? Sio mara ya kwanza Hilo wazo na Wachina wamejenga daraja huko kwao la zaidi ya km 60 ,tutawatumia hao hao kujenga umbali huo usiozidi km 50
Lini hiyo, au ni day dreams? Hilo la Busisi lenyewe lina kilomita chache ndio huko kujikongoja, itakuwa hilo la Zanzibar? Au ilikuwa story za kubembelezea mtoto anywe uji?
 
Chawa msomi katika ubora wake hawezi sema mradi huu utakuwa mzigo mzito kwa taifa, hivyo bora ferry na meli za wawekezaji sekta ya binafsi ziendelee kuwa miundombinu ya kusafirisha abiria baina ya Tanganyika na Zanzibar
Wewe nyumbu,China imejenga sana miradi kama hii.

Huu mradi utakuwa wa PPP na wawekezaji wamekuwa wakitoa hili pendekwzo siku nyingi sana.

Maelfu ya Watalii watashika Dar au Zanzibar then wata cross Kwa Barabara via hii so itakuwa poa sana
 
Lini hiyo, au ni day dreams? Hilo la Busisi lenyewe lina kilomita chache ndio huko kujikongoja, itakuwa hilo la Zanzibar? Au ilikuwa story za kubembelezea mtoto anywe uji?
Ni Suala la kufanya maamuzi na Kupitisha kama mradi wa uwekezaji wa ubia na kutangaza.
 
Wewe nyumbu,China imejenga sana miradi kama hii.

Huu mradi utakuwa wa PPP na wawekezaji wamekuwa wakitoa hili pendekwzo siku nyingi sana.

Maelfu ya Watalii watashika Dar au Zanzibar then wata cross Kwa Barabara via hii so itakuwa poa sana

Acha kabisa kuigiza nchi kubwa, taifa litaangamia kwa madeni ya taifa.

Taifa la China wana uwezo kukamilisha mradi wowote wa ndani kwa kutumia zege, nondo, benki za kichina, utaalamu n.k wanajitegemea wenyewe asilimia 100 wakati sisi vitu hivyo tutatumia trilioni za shilingi katika fedha za kigeni Dola za Marekani pia benki zetu za ndani CRDB, NBC, NMB n.k wala BoT hazina uwezo wala ubavu wa kugharamia miradi mikubwa maana zitafilisika...

Kitachotokea ni mzigo usiohimilika wa upungufu wa dola, thamani ya shilingi kuporomoka, deni la taifa ktk fedha za kigeni kuongezeka na hatimaye nchi yetu kushindwa kulipa madeni mwishowe kupigwa rehani na waChina tuwapatie kipande cha nchi ya Tanganyika maana Zanzibar haiwezi kukubali mzigo huu maana madeni yote yanadhaminiwa na Tanganyika, kesi ya DP World Zanzibar kuficha bandari zake zote.

Cheki mradi wa reli SGR unavyotusumbua : Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika
 
Litajengwa Kwa njia ya PPP yaani linajengwa na private sector so litakuwa la kulipia
Kuna wakati baadhi ya wafanya biashara huingilia kuhujumu miradi ya Serikali, nafikiri kwenye huu Mradi hatua za tahadhali zichukuliwe mapema.

Mradi usije kuishia kwenye Makaratasi, maana Kuna watu wamewekeza fedha zao kwenye biashara za boat
 
Back
Top Bottom