tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imebainisha vigezo vitano muhimu vitakavyotumika katika kuchagua sekta za kimageuzi, hasa kwa ajili ya kuchochea kipato na kuongeza ajira kwa vijana, akisisitiza kuwa utekelezaji wa vigezo hivyo ni msingi wa kuvutia uwekezaji na kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini.
Soma pia: Prof. Kitila: Serikali yatangaza mikakati 8 ya kupanua ajira kwa vijana
Prof. Kitila ameyasema hayo leo Ijumaa jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Watoa Huduma katika sekta ya uwekezaji na Kongamano la Uwekezaji lililoratibiwa na TISEZA.
Prof. Kitila ameeleza kuwa vigezo hivyo ni uwezo wa sekta kuzalisha ajira kwa wingi, hususan kwa vijana, uwezo wa kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi (export potential), nafasi ya sekta katika kukua na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine, nafasi ya sekta katika kuongeza thamani (value addition) na fursa ya sekta katika kukuza mapato ya Serikali.
Amesema Bodi ya Wakurugenzi ya TISEZA imepewa jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba vigezo hivyo vinatumika ipasavyo katika kuchagua maeneo ya uwekezaji na katika kupendekeza vivutio vya uwekezaji.
Prof. Kitila ameongeza kuwa, katika kuimarisha mazingira ya kuchochea uwekezaji nchini, ni muhimu kuhakikisha kuwa uwekezaji unalenga kujibu changamoto za kiuchumi zinazokabili nchi kwa kuzingatia vipaumbele vya Dira 2050 ambavyo vinatoa mwelekeo wa mageuzi ya kiuchumi kwa miongo ijayo.
Amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji na ameiomba TISEZA kuwa mshauri wa karibu wa Serikali na wadau katika kuhakikisha kwamba Tanzania inabaki kuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje.