Prof. Kitila: Watu wafanye kazi zao. Msimamo wa Rais Samia ndiyo msimamo wangu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakati akizungumza katka mahojiano yaliyorushwa Julai 8, 2026 na M & S Podcast


Your browser is not able to display this video.

"Kwa hiyo watu wafanye kazi zao, na usimlaumu mtu kwa kufanya kazi yake. Sasa mtu anamlaumu Kitila chuo kikuu... sasa mimi sipo chuo kikuu sasa hivi. Siyo? Mimi sasa hivi ni waziri.

Kazi yangu ya msingi ni mbili; wananchi wangu jimbo la Ubungo, pili mimi ni msemaji wa serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa hiyo msimamo wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo msimamo wangu mimi.

Na tatu, mimi sasa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi na siyo tu mwanachama, ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, alafu nilipata heshima ya kuwa mwenyekiti wa kuandika ilani. Kwa hiyo mimi sasa hivi sasa, lazima nitetee msimamo wa Chama cha Mapinduzi. Sasa unataka mimi niwe naongea kama wa CHADEMA hapa? Sasa kwenye ngoja tuyaelewe muktadha, nataka Salma aelewe muktadha. Kwa hiyo nikiwa chuoni mimi nilikuwa mwanachama wa CHADEMA, kwa hiyo unataka sasa hivi nikae CHADEMA. Mimi hapa nakaa CCM, nakaa kiwaziri, nakaa mbunge wa jimbo la Ubungo, ndiyo kazi yangu niliyonayo kwa sasa."

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…