Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Musoma: Mkinipa kura za kutosha nikawa Rais, nitasimamia Elimu Bora na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Musoma: Mkinipa kura za kutosha nikawa Rais, nitasimamia Elimu Bora na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20201006-201515.png
MKINIPA KURA ZA KUTOSHA OKTOBA 28, NA NIKAWA RAIS NITASIMAMIA ELIMU BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO "PROF.LIPUMBA"

MUSOMA- MARA

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu bora ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kila raia atahimizwa kujiendeleza kielimu hasa kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano.

Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa na CUF itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza kielimu wasichana na kujenga misingi imara ya kuendeleza elimu za hisabati, sayansi na teknolojia.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kwamba ifikapo 2025 asilimia 50 ya Shule za Umma nchini zinakuwa na Uwezo wa Kufundisha wanafunzi wake kwa njia ya TEHAMA na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hili litawezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo hata pale shule zitakapofungwa kwa dharura kama tulivyojifunza kupitia janga la CORONA.
 
Back
Top Bottom