Prof. Lipumba amdai IGP Sirro saa yake

Prof. Lipumba amdai IGP Sirro saa yake

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
images (49).jpeg

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGPSimon Sirro kuitafuta saa yake ya mkononi aliyonyang'anywana askari wake wakati wa mvutano ulioibuka karibuni.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho na wananchi mkoani Tabora, Lipumba amelishutumu jeshi hilo kwa kuvuruga shughuli za chama hicho zilizopangwa kufanyika, ikiwemo uziunduzi wa mashina katika kata za Mbugani na Mapambano pamoja na kuchangia damu.

Amesema polisi waliwazuia kufanyia shughuli hiyo kwenye ofisi zao, badala yake wafanyie kwenye ukumbi, na kwamba mwishoni walifanikiwa kuchangia chupa 20.

Amesema atamshauri Rais atembee kwenye kauli zake zakutetea demokrasia ya kweli, yenye msingi wa maendeleo pamoja na kulinda heshima na utu wa Watanzania.

Ameongeza kuwa haki ni muhimu kwani itawezesha wananchi kufanya kazi kwa uhuru, hivyo kujiletea maendeleo na kwamba Rais atakumbukwa na kujipatia heshima kutokana na kusimamia kauli yake, na kwamba akija kugombea tena kazi inakuwa nyepesi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16] nchi ina njaa hii,
Waachiwe majini wararurane
 
Kumbe bwana huyu yupo?????

Mama Samoa maanisha Basi kauli zako!!!
Yaana mafaraka ni sawa na madawa ya kulevya.
Mama Samia anaona jinsi mwenda kuzimu anavyo laumiwa na kusutwa kwa aliyo watendea watu.
Lakini bado haoni maana ya kujiandalia maisha mema ya baadae.. Bado nae ana fuata ujinga wa mwenda kuzimu.
Ndipo ninapo amni ni vugumu sana hawa watu kuionja pepo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16] nchi ina njaa hii,
Waachiwe majini wararurane
 
Hivi huyu bwana hata mahakamani au ukonga kumjulia hali Mbowe na wenzake amewahi kutimba?
 
Back
Top Bottom