Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba amshukia vikali Tundu Lissu, ahoji kuweka pingamizi kwa wagombea wawili ilhali wote wamefata maelekezo ya Tume

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lissu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera, Amani, Maendeleo na Demokrasia ya Nchi yetu.

Prof. Lipumba amehoji sababu za Lissu kumuwekea pingamizi kwenye tume ya uchaguzi eti kisa tu amefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi!! Lipumba amehoji asipofuata maelekezo ya tume ya uchaguzi afuate maelekezo ya nani?? Pia amehoji wagombea wote wa urais mwaka huu wamefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi akiwemo Membe, iweje awawekee pingamizi wagombea wawili tu?

Hali hiyo imemsikitisha sana Lipumba na kuwaasa watanzania kutokumchagua Lissu kwani ameonyesha udikteta wa kuminya demokrasia mapema sana.

Your browser is not able to display this video.

 
Mgombea urais wa Cuf ,Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lisu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera ,amani , maendeleo na democrasia ya nchi yetu...

Maelezo yake tu ya mwisho hapa yameshatusaidia kuwa kumbe ni kweli yupo katika 'Payroll' ya CCM na Serikali yake nzima iliyo chini ya Rais JPM.
 
Mgombea urais wa Cuf ,Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lisu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera ,amani , maendeleo na democrasia ya nchi yetu...

Yale yale ya 2015 kwa kumuita Mhe Lowassa fisadi halafu kakimbilia Rwanda kutaliiiii! CUF, ACT Wazalendo, TLP, NCCR, ADC, CHAUMA, UPD, TADEA, hawapati mbunge hata mmoja Tanzania Bara na Chadema hawapati mbunge hata mmoja Tanzania Visiwani!! Act Wazalendo watapata wabunge wanne tu Visiwani! Procrastination. hiyo.
 
Lisu amefanya makosa sana, kitendo tu cha kumtaja Lipumba kimefanya watu wajue kuwa hata Lipumba anagombea urais.
Kumbe ulikuwa unaona ni sawa watu kutokujua kuwa hadi Lipumba nae anagombea urais ila hauoni sawa vyombo vya habari vinavyompotezea Lissu!
 
Mgombea urais wa Cuf ,Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lisu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera ,amani , maendeleo na democrasia ya nchi yetu...
Profesa Lipumbaaaa katika ubora wake
 
Mbona Lissu alisema wazi kuna wengine kaamua kutowawekea mapingamizi?
Kwanini hakuweka kama wote walifanya kosa moja. Nyie jamaa Lisu wenu kawashikia akili yaani you are not using your brain kabisa
Mahaba yanawafanya mnakuwa fools. jamaa kakosea kuweka mapingamizi ambayo actually hayana mantiki
 
Kumbe ulikuwa unaona ni sawa watu kutokujua kuwa hadi Lipumba nae anagombea urais ila hauoni sawa vyombo vya habari vinavyompotezea Lissu!

Lissu ni kama moto, hata usipouona utasikia harufu yake. Huyo Lisu hata asipotangazwa na chombo chochote cha habari humu nchini, bado habari zake watu watazitafuta.

Mpaka sasa Tundu Lisu hapewi covarage na vyombo rasmi vya habari, na hata akipewa ni zile negative, lakini ndio mwenye mvuto automatically kwa watu.

Huo ndio ukweli usiopingika. Huyo Lipumba acha tu kupewa covarage na vyombo vya habari, hata awe mtangazaji kwenye media zote au mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hana mvuto tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…