PostGE2025 Prof. Lipumba ataka Serikali ya Mpito kusimamia Maridhiano na Katiba Mpya. Aikataa tume ya Chande

PostGE2025 Prof. Lipumba ataka Serikali ya Mpito kusimamia Maridhiano na Katiba Mpya. Aikataa tume ya Chande

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Si kweli yeye ndio chanzo cha kuvuruga CUF kwa mipango na srikali
Hawa ni wale ''wanasiasa'' wanaoenda kulingana na upepo. Huyu alihusika sana kumvuruga marehemu Seif na CUF, na huenda alikwamisha mabadiliko ambayo ungekuta yameshatokea. Juzi juzi CCM wamemnyang'anya uenyekiti wa CUF waliokuwa wamempa baada ya ule mgogoro. Leo anaibuka baada ya kutumika na kutupwa.
 
Au Lipumba anataka kuhamia Chadema anatupanga? Mbona katoa hoja nzito sana ambayo ndiyo suluhusisho la kweli.

Haya Tundu Lissu akitolewa kwa sharti la mazungumzo kisha akaweka msimo huu, kuna tatizo?
 
Ibrahim Lipumba ataka Serikali ya Mpito kusimamia Maridhiano na Katiba Mpya. Aikataa tume ya Chande.

Lipumba amesema Tume ya Chande ilienda kufanya kazi ambayo majibu yashatoka.

Amesema Mama Samia alisema watu walipewa fedha, Watu walitaka kupundua Serikali nk. Sasa kama chanzo cha vurugu alijua kwanini aunde Tume?

Kwamba CCM. sio chama cha siasa bali chama dola cha katiba ya 1977 ambayo inaweza kumfanya samia kuwa Dikteta. CCM hawawezi kutupa katiba mpya.

Nchi tajirii watu wake Masikini. Kasema

View attachment 3575086
Well said..
 
Hawa ndio waliopewa kibaba cha mwisho ndani ya ghala wakahemee ili kijiji kilichokumbwa na njaa kiepuke janga; badala yake ndio wakakididimiza moja kwa moja!

Tanzania imefika hapa tulipofikia leo kwa sababu ya watu wa aina ya huyu, wasiokuwa na uchungu wowote na taifa lao.
 
Aliingiziwa 1B kwenye acc yake ili aidhoofishe CUF.. Akaenda Kariakoo akaoneshwa ghorofa wakati akiwa kwenye mchakato wa kulipa akaambiwa amechaguliwa kuwa mmojawapo wa waangalizi wa uchaguzi wa Rwanda toka Tanganyika
Hivyo anaweza kutoa advance ya kishika uchumba halafu akirudi anamalizia mchakato

Akapewa mkataba wa awali uliokuwa na kipengele cha kutorudisha advance kama akishindwa kumalizia malipo (hakuwa na shaka kwakuwa mzigo ulikuwa umetulia bank)

Akapewa VIP treatment kwenda Rwanda na kurudi Tanganyika baada ya uchaguzi kumalizika

Baada ya kurudi akatulia siku 2 ili ya 3 aende akakamilishe mchakato wa kumiliki mjengo Kariakoo

Lahaula kufika bank account inasoma sifuri na ina deni la service charge🤣🙌🏿
Kutaka kufuatilia advance akakumbuka alisaini mkataba wa kutorudishiwa advance biashara ikishindikana😂🙌🏿

Mchezo mzima ulichezwa na vijana wa jiwe😂
Nitaanzia wapi mimi kupinga stori kama hii!

Hii nchi yamefanyika madudu ya kila aina; kama watu maelfu kuuliwa, na walioua wanafanya kila liwezekanalo kusahaulisha waTanzania tukio hilo la kusikitisha kwa kuwaonyesha sura za huruma za "kuasili" akina 'Grace Samia Suluhu Hassan!

Kuna komedi kubwa zaidi ya hiyo?
 
Back
Top Bottom