Ndio Lipumba yupo kwenye mstari na anaposema aliyosema Rostam ni mazito ,hivi tatizo lipo wapi ? wewe unaejua kuwa Mengi yupo katika haki ni wewe tu .ila waTz walio wengi wanamuona Mengi kuwa ni mwizi aliekubuhu au jambazi sugu ,sasa alichofanya Lipumba ni sawa na kumwambia Mengi jisafishe ? Na tumeona ametokeza kwa mara ya pili kukanusha kwa vielelezo huku ni kujisafisha , Inaionyesha mna matatizo ya kufahamu Lecture jamani kwenye vyuo vikuu hakuandikwi ubaoni ,yaani mnaonekana kama mnaazima magazeti na kusoma tu na halafu mnakurupukia hapa JF.
Kumfahamu Lipumba kunataka mtu msomi ambae amezoea kusikiliza Lecture na kuondoka na kina cha yaliyozungumzwa ,kuna watu wanapata tabu sana wafikapo vyuo vikuu vya nchi za ughaibuni ,jamani wanaotoa lecture huko ni maprofesor ambao humwambii kukamata chaki akaujazia notice kwenye ubao ,just anaingia na kukufahamisha mawili matatu ,na saa ingine anawapa kurasa za kitabu mkasome siku ya pili akiingia anauliza kama kuna mtu hajafahamu ,na akitokea anakwambia mfuate ofisini na wiki ijayo mtihani.
Lipumba ni mmoja ya mtu ambae inataka umfahamu kwa kina na kama una muda uyaangalie mazungumzo yake mstari kwa mstari ,ila kama ni wasomaji mnaokimbilia na kufukuzana na njaa mtapata tabu sana.