CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
HANDENI VIJIJINI
Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa
Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu bora ya msingi, elimu ya
sekondari na elimu ya juu. Kila raia atahimizwa kujiendeleza kielimu hasa
kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano.
Serikali ya umoja wa
kitaifa itakayoundwa na CUF itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza
kielimu wasichana na kujenga misingi imara ya kuendeleza elimu za hisabati,
sayansi na teknolojia.
Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha
kwamba ifikapo 2025 asilimia 50 ya Shule za Umma nchini zinakuwa na
Uwezo wa Kufundisha wanafunzi wake kwa njia ya TEHAMA na asilimia 100
ifikapo 2028.
Hili litawezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo hata
pale shule zitakapofungwa kwa dharura kama tulivyojifunza kupitia janga la
CORONA.