Uchaguzi 2020 Prof.Lipumba, Handeni: Mkinipa kura za kutosha Oktoba 28, na nikawa rais nitasimamia elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
MKINIPA KURA ZA KUTOSHA OKTOBA 28, NA NIKAWA RAIS NITASIMAMIA ELIMU BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO "PROF.LIPUMBA"

HANDENI VIJIJINI

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa
Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu bora ya msingi, elimu ya
sekondari na elimu ya juu. Kila raia atahimizwa kujiendeleza kielimu hasa
kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano.

Serikali ya umoja wa
kitaifa itakayoundwa na CUF itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza
kielimu wasichana na kujenga misingi imara ya kuendeleza elimu za hisabati,
sayansi na teknolojia.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha
kwamba ifikapo 2025 asilimia 50 ya Shule za Umma nchini zinakuwa na
Uwezo wa Kufundisha wanafunzi wake kwa njia ya TEHAMA na asilimia 100
ifikapo 2028.

Hili litawezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo hata
pale shule zitakapofungwa kwa dharura kama tulivyojifunza kupitia janga la
CORONA.
 
Lipumba yuko vizuri kuliko Mbowe na genge lake la vibaraka. Ni mara 100 mtu achague CUF, kuliko chama cha faru John.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…