Prof. Lipumba: Kuna vyama vina sera za kutongoza mademu

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Prof. Lipumba: Hitimisho, baraza kuu linatoa wito kwa watanzania pamoja na waandishi wa habari kujiunga na chama cha CUF chenye lengo la kujenga nchi yenye haki sawa na furaha kwa wananchi wote. Kitakachotumia rasilimali za nchi yetu kukuza uchumi unaoongeza ajira utakaowapa na kuwanufaisha wananchi wote, kitakachoimarisha uwajibikaji na kujenga mfumo endelevu wa kupambana na rushwa na ufisadi.

Vyuma vinazidi kukaza, tujiunge na kuimarisha CUF ili hatimaye tupate grisi ya vyuma vilivyokaza na kuna vyama vingine vina sera ya kutongoza mademu, sisi tuna sera ya kujenga nchi yenye haki sawa na furaha kwa wananchi wote.

Your browser is not able to display this video.
 
Dah...Anakisema kile Chama waziwazi hivi......Professor sio mambo mazuri hayo.....
 
Mwizi mkubwa. Ulidanganywa uka uza utu wako. Bora watingoza mademu wenye msimamo kuliko wewe mnafiki ulie uza hadhi na utu wako ili kuua upinzani
 
Distinguished Professor anaongelea sentensi ya rejareja jukwaani anaita sera.

Usihadaike na akili za darasani mkuu,
Ukiambiwa alikuwaga Tanzania One form six na GPA ya 5 UDSM na Masters alisoma Stanford university hawez amini.
Njaa mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…