Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Potelea mbali tu hatawakijua

Potelea mbali hata wakijua sio hatar ila cha muhim kujua n kwamba bill zang nalipa mwenyewe
 
profesa anaweza kuwa hayuko sahihi.

pepa ina pande mbili - kipande chembamba cha juu chenye visanduku vya kuandika namba na kipande kikubwa cha chini chenye picha za wagombea. zinapotenganishwa, kile kipande cha juu kinabaki na huyo karani, mpiga kura anaondoka na kipande cha chini chenye picha ya wagombea tu kwa ajili ya kuenda KUPIGA SPANA kwenye kizimba.

kwa muktadha huo unawezakujua ni nani nanani wamepiga kura lakini ni vigumu kujua nani kampigia nani?

magufuli chaliii.
 
Ni kweli aisee hata mimi hicho kitu nimekiona lkn nikajua ndio utaratibu wa mwaka huu..ila poa tu wala asitutishe Magufuli maana hawezi kuongoza milele ipo siku yake tu na yeye atalamba Udongo
 
Mimi niliuliza karani kwa nini unaandika namba yangu ya kadi ya kupiga kwenye karatasi wakati kura ni siri yangu.Jibu ni hivi,karatasi ya kupiga haina namba ya kumbukumbu (SERIAL NO) ila kwenye kitabu wanakochana pale kwenye shina ndipo kuna serial number.Namba ya kadi yako inaandikwa pale kwenye shina la kitabu.Kwa upande fulani ni nzuri kama kutatokea tatizo la kuhakiki idadi ya wapiga kura!
 

Katiba yeti ni tatizo kubwa, ila kwa rais tuliye naye tatizo hilo limekuwa wazi zaidi.
 
Potelea mbali tu hatawakijua

Potelea mbali hata wakijua sio hatar ila cha muhim kujua n kwamba bill zang nalipa mwenyewe

Usichukulie poa bro!
Hivi unajua maana ya KURA YA SIRI?
Kuna madhara yanayoweza kutokea kama watajua umepiga against the incumbent president hasa ukiwa Mtumishi wa Umma, Mfanyabiashara na hata raia tu!!!. Wanaweza kukufuatilia wakaku shughulikia kwa ule mtindo wa "Watu wasiojulikana".....!!!
Huu Utawala siyo kabisa!
 
Prof Lipumba amesema kweli. Hili swala liangaliwe in the future.
 
Kuna muda ukiongea jambo fulani watu wanahisi 'there is something wrong in your mind'
Yaan tangu 1995 unapambana kwenye hamna.

Ni vizuri ukubali muda umekupita
Hivi hili jibu linaendana au kujibu tuhuma / issue aliyoelezea ? Angalia issue aliyo-raise majibu uliyotoa wewe alafu tafakari kwa mujibu wa hizo statement mbili ni nani hapo ana walakini kwenye mind yake...
 
kmmk inaonyesha watu watashughulikiwa mmoja mmoja. Hivi ndo tumefikia hapa kweli? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Mzee arudi chato tu kwa kweli.
 
Kwa iyo yeye alitaka amchague Lissu, huku akitegemea uteuzi wa JPM?!
 
Hivyo vitisho tu Hasa kwa watumishi. Lkn kwetu hilo hakipo. Tumepiga tu, karani kajaza karatasi mezani nyingi, ukifika anakupa ya Diwani na Rais. Kwetu Mbunge hakutuendea Haki. Natamani nimpigie hata ya hapana tu. Kupita bila kupingwa ni mpango wa shetani
 
Asante kwa kushiriki upuuzi na kumnadi yule mpuuzi mwenzio
Huu uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine, na ndio maana watanzania wengi wamepuuza zoezi zima. Idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo kwenye vituo. Mambo kama hayo nani yuko tayari kwenda kushiriki huo upuuzi?
 
Huu utaratibu toka 1995 ina maana alikuwa hafuatilii
 
Nivizuri namba ya mpiga kura kurekodiwa katika vishina vinavyo baki baada ya karatasi ya kupigia kura kuachanishwa hii itasaidia wakati wa kuhesabu ikionekana kura zimezidi kuliko idadi halisi ya waliopiga watapta uhakika wakihesabu vishina ambavyo ilikatwa karatasi halisi. Na ikitokea idadi znatofautiana ina maana zote kwenye sanduku ilo zimeharibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…