Maswali kwa simu:-
Muuliza swali 1. anadai anawakubali sana Dr Slaa na Pro. Lipumba anachosema kwa nini wasingeungana ili waweze kufanya mapinduzi makubwa na ya nguvu?
Jibu: Tatizo vyama vingine vilisema wanaenda majimboni, Slaa, Mbowe, Mrema sasa tulijua hakuna mtu anayetaka kusimama na sisi tulisha jipanga, lakini next time tunaweza kufanya hivyo, lakini vile vile katiba inasumbua hapo inabidi kusajili chama kiwe chama kimoja, kwa hiyo katiba inabidi ibadilike, ili kulinda madiwani na wabunge..kalifafanua vizuri sana.
Jibu: Kabla hata ya katiba mpya vyama vilikuwa vinaruhusiwa kuunganisha vyama bila wabunge na madiwani kupoteza nafasi zao, lakini katiba yetu imechakachulia kuifanya iwe vigumu kwa vyama vya upinzani.
Muuliza swali 2. Powatila hazifai kwa kilimo kulingana na ardhi yetu, serikali imepoteza pesa nyingi na gharama kubwa je akiingia madarakani atawaadhibu vipi watu wanaonunua vitu visivyo na tija na kuingiza serikali hasara kubwa?.
Jibu: Serikali inaingiza watu mkenge, inakurupuka bila kufanya utafiti ni kama shule za kata na hivyo kutuingiza gharama kubwa
Muuliza swali 3. Namkubali sana Pro.Lipumba, viongozi waliotangulia inabidi wawe mfano kwetu, naomba vyama vya upinzani waungane kama kenya, maghembe amedai hakuna kuchija wanafunzi mpaka form four, je tumefikia huko?
Jibu: Mitihani ya darasa la saba ni muhimu, watatenga 25% kwenda kwenye elimu, kodi inapotea tuna hela nyingi mfumo wa kodi ni mmbaya na ukusanyaji ni mbovu.