Bado unashikilia vitu vya kubuni kwa akili yako...Mkuu hakuna makubaliano ya Prof. Lipumba na Kikwete.
Ahaaaa! sasa nimekuelewa ulikuwa unanishughulisha sana, kumbe unaongea mambo ya JF? Mkuu, humu jukwaani kila mtu ana namna ya kukereketwa kwake, haina maana ukereketwa wa mtu na ushabiki wake humu JF ndiyo ukaufanya kuwa msimamo wa chama.
Mimi binafsi nakerwa na viongozi wabovu wanaoharibu harakati za vyama vya upinzani (Mfano Mrema na Mbowe) hii haina maana kuwa ndiyo msimamo wa chama changu. Kama washabiki wa CUF ndani ya JF wanaiponda chadema huo ni ushabiki wa kivyama na siyo msimamo wa chama cha CUF.
Mkuu nina hakika kuwa tangu CUF iingie katika ushindani wa kisiasa imekuwa ikijipanga vizuri na haikuhitaji msaada wa chama chochote kusimama kwanye uchaguzi. Kama chama chochote kingine kikisema kuwa kinaunga mkono CUF, haitakuwa na maana kuwa tumekubaliana hivyo kama makubaliano hayo hayapo.
Nitakupa mfano, mwaka huu chadema wamesema wanaunga mkono CUF kwa kiti cha urais wa Zanzibar, wala hakuna makubaliano hayo! kwamaana hata kama wasingesema CUF inaweza kusimama bila ya kuungwa mkono na chama chochote.
Hivyo hata mwaka huu tusingekuwa na haja ya kusubiri chadema tujuwe wana mgombea au hawana ndiyo tukubaliane kuungana mkono wakati mchakato huo haukuandaliwa tokea hapo. CUF haiwezi kufanya mambo kwa kukurupuka ndiyo maana imeweza kupiga hatua kubwa kuidhibiti CCM kila kona.