Pre GE2025 Prof. Lipumba: Tumeshajeruhiwa na Muungano wa Vyama vya Upinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa maridhiano ndani ya vyama vya upinzani yamekuwa yakileta madhara na kuwajeruhi, na kwamba wamejifunza kutokana na yaliyotokea kipindi cha nyuma.

1740984016117.png
Akizungumza na Wanahabari Lipumba amesema kuwa kuna watu wanaotafuta madaraka kwa maslahi binafsi badala ya kujenga demokrasia ya kweli.

Amesema kuwa mwaka 2020, alikumbana na hali ya kushangaza ambapo alijitokeza kugombea urais, lakini alikumbana na pingamizi la dakika za mwisho kutoka kwa Tundu Lissu, jambo ambalo alidai lilikuwa kinyume na misingi ya demokrasia.

Soma, Pia: Chadema yapigilia msumari masharti ya kushiriki kwao, wakisisitiza 'No reform, no election'

Lipumba amesema kuwa ingawa alikamilisha taratibu zote za kisheria, alikumbana na kikwazo cha kisiasa kilichotokana na Mpinzani mwenzake ambaye alikuwa Mgombea Urais wakati huo kupitia Chadema Tundu Lissu

"Sasa ukishajua kwamba umegongwa, umeumwa lazima uwe na tahadhari, kuna watu ambao wanatafuta madaraka sio kujenga demokrasia.wapo kama Trump kwamba ukishaingia basi uanze kuwashughulikia wote, lazima tuwe macho katika hili kwa sababu tushagongwa gangwa sana" amesema Lipumba.

Prof. Lipumba ameongeza kuwa katika historia ya siasa za upinzani, vyama vimekuwa vikishirikiana kwa makubaliano ya muda mfupi, lakini mara nyingi hayo yamevurugwa kutokana na kutokuwa na umoja wa kweli. Akirejelea uchaguzi wa 2014, alikumbusha jinsi baadhi ya vyama vilivyokuwa vikitumia udhaifu wa vyama vingine kujinufaisha.

Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha demokrasia inakua nchini, vyama vya upinzani vinapaswa kuwa na maridhiano ya kweli na ya kudumu, badala ya kuingiza maslahi binafsi katika vikao vyao.

"Mifumo isiyo huru tulikubaliana kabisa sasa mnafanyeje pasina kuwa na maridhiano, sasa ukiwa unahitaji unatoa wito kwamba tufanye maridhiano, tufanye mazungumzo tukae katika kikao cha pamoja.sasa ikiwa ndo wito wako huo ukaweka tu kama hatukai kwenye kikao cha pamoja hili na hili, moja kwa moja unaonekana kwamba hauhitaji kuwa na maridhiano."

"Katika masuala ya kidiplomasia inabidi nondo zako zingine uziweke akiba.kama utakwenda na kauli mbiu kwamba tutaicheza ngoma kwa Kadri itakavyodundwa basi hiyo msitoe mapema iweke akiba.lakini pia uwaandae watu"
amesisitiza Lipumba

CHANZO: Jambo TV
 
Usizunguuke profesa sema tu ukweli huwaamini chadema kwa kile wakichofanya kubadili gia angani na kumleta lowassa!
 
Alafu unakuta wapinzani wa kawaida wanamatumaini na kariba ya upinzani tulionano Tanzania... CCM ipo ipo sana, mpaka kife kwanza kizazi chote cha Mziwanda..
 
Usizunguuke profesa sema tu ukweli huwaamini chadema kwa kile wakichofanya kubadili gia angani na kumleta lowassa!
Huenda umesahau. CUF waliunga mkono ujio wa Lowassa CDM na walimuweka Haji Duni kuwa mgombea mwenza aliyehamia CDM kwa lengo la maslahi ya CUF katika huo muunganiko.

Lipumba anazungumzia 2020, Lowassa aligombea 2015
 
Ameona haya kusema 2015 sababu hiyo ilimfanya kujitoa cuf na kukimbilia rwanda kabla ya kurudi na kuibukia ikulu shati lote mgongoni limoroa jasho na kuja kuiteka cuf na kuifanya mali yake akimpora maalimu seif!
 
Akawa analala ofisi za CUF Buguruni, ukipita asubuhi unamuona anaswaki kwenye balcony,
Mzee mpuuzi sana yeye na Sakaya ndio chanzo cha CUF kufa, na kuhamia ACT
 
Hawa akina Lipumba ni Ccm na hawana wanachopigania Chenye Tija Kwa ajili ya demokrasia wala nchi✊🏿
Kwani kuna anayepigania?.Wanasiasa ni hawa hawa hakuna mpya.wote wanawaza maslahi binafsi.Hao unaofikiri wanapigania demokrasia nikwasababu hawajapata buyu la asali.Siku wakilipata hutasikia chochote.
 
Mtikila namkubali,ndio Pruto wa siasa za Tanganyika,alitaka tuwe na mgombea binafsi kisheria akashinda kesi mahakama kuu.
Akita wagombea nyadhifa hizo wawatumikie wananchi wao badala ya kuwa tu watiifu kwa chama.
Kuna watu wanajitambulisha kana kwamba ni wapigania haki za wananchi kumbe wanapigania matumbo yao kwa kutumia kivuli cha vyama vya siasa.
Wamechelewa na hawakubaliki watafute kazi nyingine.Na sisi hatudanganyiki
 
Kwani kuna anayepigania?.Wanasiasa ni hawa hawa hakuna mpya.wote wanawaza maslahi binafsi.Hao unaofikiri wanapigania demokrasia nikwasababu hawajapata buyu la asali.Siku wakilipata hutasikia chochote.
Ni kwa mawazo mgando kama haya ndiyo maana hatutafanikiwa kama taifa kupiga hatua kubwa za kinaendeleo. Kuna watu wameamua kuifia nchi tofauti na mawazo yako. Kwa mifumo ya kiutawala, viongozi wa nchi huwa ndiyo 'icon of the nation' lakini hawapaswi kujiangalia kwa maslahi yao tu. Kiongozi lazima umuone kila raia wa nchi yako kuwa ana thamani sawa na yako na anastahili kila kilicho bora kwa ustawi wa maisha yake na taifa kwa ujumla. Ndiyo maana watu wenye uelewa mpana wamekuja na slogan ya 'no reform no election'. Yaani tutengeneze play ground iliyokuwa fair kwa kila mtu kuweza kushindana bila hofu.
 
Mimi sinahamu na lipumba alivyo mupindua Maalim au kigaidi akajitoa uenyeketi akarudi kwa mapinnduzi ya kishenzi akaivuruga CUF huyu hafai kabisa na haamiki ni kigeugeu angalia alivyo igawa CuF au kuivunja CuF ni mushenzi wa siasa
Hapendi wa Tanzania anapenda kuwa Mwenyekiki ana roho ya Idiamin Dada hafai hafai ni mudini huyu ni mwenda wazimu tu anaweza kumwamini Lipumba Munyamwezi msomi ila Mpumbavu asiye na amani ukweli mambo ya maalimu yanatoa majonzi alivyo fanya ,mwacheni awe peke yake watanzania Lipumba hatufai kabisa . Let him lost and die fool can't be trusted never ever
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa maridhiano ndani ya vyama vya upinzani yamekuwa yakileta madhara na kuwajeruhi, na kwamba wamejifunza kutokana na yaliyotokea kipindi cha nyuma.

Akizungumza na Wanahabari Lipumba amesema kuwa kuna watu wanaotafuta madaraka kwa maslahi binafsi badala ya kujenga demokrasia ya kweli.

Amesema kuwa mwaka 2020, alikumbana na hali ya kushangaza ambapo alijitokeza kugombea urais, lakini alikumbana na pingamizi la dakika za mwisho kutoka kwa Tundu Lissu, jambo ambalo alidai lilikuwa kinyume na misingi ya demokrasia.

Soma, Pia: Chadema yapigilia msumari masharti ya kushiriki kwao, wakisisitiza 'No reform, no election'

Lipumba amesema kuwa ingawa alikamilisha taratibu zote za kisheria, alikumbana na kikwazo cha kisiasa kilichotokana na Mpinzani mwenzake ambaye alikuwa Mgombea Urais wakati huo kupitia Chadema Tundu Lissu

"Sasa ukishajua kwamba umegongwa, umeumwa lazima uwe na tahadhari, kuna watu ambao wanatafuta madaraka sio kujenga demokrasia.wapo kama Trump kwamba ukishaingia basi uanze kuwashughulikia wote, lazima tuwe macho katika hili kwa sababu tushagongwa gangwa sana" amesema Lipumba.

Prof. Lipumba ameongeza kuwa katika historia ya siasa za upinzani, vyama vimekuwa vikishirikiana kwa makubaliano ya muda mfupi, lakini mara nyingi hayo yamevurugwa kutokana na kutokuwa na umoja wa kweli. Akirejelea uchaguzi wa 2014, alikumbusha jinsi baadhi ya vyama vilivyokuwa vikitumia udhaifu wa vyama vingine kujinufaisha.

Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha demokrasia inakua nchini, vyama vya upinzani vinapaswa kuwa na maridhiano ya kweli na ya kudumu, badala ya kuingiza maslahi binafsi katika vikao vyao.

"Mifumo isiyo huru tulikubaliana kabisa sasa mnafanyeje pasina kuwa na maridhiano, sasa ukiwa unahitaji unatoa wito kwamba tufanye maridhiano, tufanye mazungumzo tukae katika kikao cha pamoja.sasa ikiwa ndo wito wako huo ukaweka tu kama hatukai kwenye kikao cha pamoja hili na hili, moja kwa moja unaonekana kwamba hauhitaji kuwa na maridhiano."

"Katika masuala ya kidiplomasia inabidi nondo zako zingine uziweke akiba.kama utakwenda na kauli mbiu kwamba tutaicheza ngoma kwa Kadri itakavyodundwa basi hiyo msitoe mapema iweke akiba.lakini pia uwaandae watu"
amesisitiza Lipumba

CHANZO: Jambo TV
CUF Haina uwezo wa kupata hata Jimbo Moja!

Upinzani jifunzeni Kenya,wenzenu wanavyofanya!
 
Back
Top Bottom