GE2025 Prof. Lipumba: Ukisema waliofanya uhalifu wametoka nje ni kama kutangaza mipaka haina ulinzi. Katika hali kama hiyo Rais unapwaya

GE2025 Prof. Lipumba: Ukisema waliofanya uhalifu wametoka nje ni kama kutangaza mipaka haina ulinzi. Katika hali kama hiyo Rais unapwaya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na vyombo vya habari Novemba 6, 2025, amesema kwamba kitendo cha Rais Samia kudai kuwa walifanya uhalifu ni watu kutoka nje si sawa na alipaswa kufikiria kabla ya kuvishtumu vyombo vya usalama kwa kushindwa kutazama matukio yanayokuja;

"Ukisema kwamba hawa wametoka nje ni kama vile unatagaza mipaka yetu haina ulinzi kabisa, mtu yeyote anaweza kuingia na kufanya vurugu; mambo mengine hata unapotaka kujibaraguza ebu fanya fikra kwanza kwani wakati mwingine ndiyo unazidi kujiangusha."

"Nyie mnajua mnauchaguzi, kama unausalama wa taifa wanapaswa kukujulisha kwamba kuna mbinu za watu kutoka nje kuja kufanya vurugu kwahiyo inabidi tujipange"

"Yeye [Rais Samia] kueleza hilo ni kama kutoa shutma kwamba kwa kweli hatuna Vyombo vya usalama vya kuweza kutazama matukio yanayokuja. Sasa katika hali kama hiyo Rais unapwaya"

 
Back
Top Bottom