Prof. Makame Mbarawa: Uwekezaji wa DP World, mapato yafikia TSh. Trilioni 8.26 ongezeko la asilimia 16.67

Prof. Makame Mbarawa: Uwekezaji wa DP World, mapato yafikia TSh. Trilioni 8.26 ongezeko la asilimia 16.67

Serikali imesema kitendo cha kushirikisha Sekta Binafsi katika uendeshaji wa shughuli za bandari kwa kuingia ubia na Kampuni za DP World na TEAGTL katika kuendeleza na kuendesha baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam, kumeleta mafanikio mbalimbali yakiwemo kuongezeka kwa mapato yatokanayo na Kodi ya Forodha kutokana na shughuli za kibandari, ambapo katika kipindi cha Julai, 2024 hadi Februari, 2025 jumla ya Tsh. trilioni 8.26 zimekusanywa sawa na ongezeko la Tsh. trillion 1.18 ikilinganishwa na Tsh. trilioni 7.08 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2023/24 kabla ya kushirikishwa kwa Waendeshaji binafsi katika bandari hiyo.

Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma leo May 15,2025 Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema "Faida nyingine ni kupungua kwa gharama za uendeshaji wa Bandari ya Dar es salaam kutoka Tsh. bilioni 975.01 hadi kufikia Tsh. bilioni 685.16 sawa na punguzo la asilimia 30, kupungua kwa muda wa kusubiri meli nangani kutoka wastani wa siku 46 hadi wastani wa siku saba kwa meli za mizigo mchanganyiko na kichele na meli za makasha gatini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku tatu"

"Faida nyingine ya uwekezaji huo ni kuongezeka kwa wastani wa shehena ya makasha inayohudumiwa kwa mwezi kutoka makasha (TEUs) 17,000 hadi makasha (TEUs) 25,000 sawa na ongezeko la asilimia 47, kwa ujumla hatua hii ya ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika kuendeleza na kuendesha bandari nchini, umechangia kufikiwa mapema kwa lengo la Mpango Kabambe wa TPA wa miaka 20 (2021/22 – 2044/45) ulioweka wa kuhudumia tani milioni 30 za shehena ifikapo mwaka 2029/30"

"Hata hivyo, matokeo ya uendeshaji wa bandari hadi kufikia mwezi Machi, 2025 tayari ufanisi wa uhudumiaji wa shehena wa bandari zote nchini umefikia tani milioni 27.55 na kwa mwenendo huu lengo la tani milioni 30 litafikiwa mapema sana kabla ya muda uliowekwa"
Sasa hilo ni ongezrko la maana? Na je huyo muwekezaji anakula kiasi gani? Je uhuru wetu unapungua kiasi gani kwa kuweka DPW? NA JE WENYEWE HATUNA UWEZO BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 60 YA UHURU KUENDESHA BANDARI ZETU? Kuendesha bandari sio kutengeneza ndege. Bila shaka wahindi na waarabu wameona ni zamu yao kujinufaisha na ujinga wa waafrika.
 
Ongezeko la kawaida sana, lingekuwepo bila hata DPW
 
Back
Top Bottom