Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka
Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa
Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu( economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class
Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa
Source ITV Habari