Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Aliyeenda JPM kuanzisha bwawa la mwl Nyerere lilikuwa la kuupa msukumo SGR. Sasa mmekuja na longolongo nyingine.

Majuzi mmewaambia wanaoishi ukanda wa Rufiji na Kilwa eti Wahame kutokana na athari za maji mliyoyafungulia wenyewe ya bwawa .
Kama sio mwanzo wa kuhujumu hili bwawa ni nini!
Mwisho wa siku hakutakuwepo na maji!

Hao wananchi mliowafungulia hayo maji waende wapi na je mko tayari kuwalipa fidia kwa uzembe huo?
WaTanzania msiwafanye wajinga.
Katiba mpya Katiba .
 
viongozi wetu wa kitanzania wengi wao ni vilaza sana, yaani ukitoa gari la serikali, ukatoa ofisi ya serikali, ukatoa na nyumba ya serikali...ukaviweka mbali na kiongozi, alafu ukamwambia kiongozi huyu atoe maelezo ya jambo fulani....utashangaa sana, utajiuliza amechaguliwa kwa kigezo kipi?, je ameteuliwa kwa kupakaa lotion? sura imeonekana kama kitumbua cha mchele ama sababu ipi zaidi alikuwa nayo 😛 , ukimchukua dogo wa form II wa shule ya kata si atakupa sababu za namna hiyo? kuna haja jitu zima lizungumze kama mwanafunzi??🙁
 
Prof. Mbarawa kashiindwa kuweka wazi au kufafanua hili suala la hii SGR, lakini alivyosema ni kweli. Treni zinazokwenda kwa kasi Duniani, kuanzia namba moja mpaka namba tatu zipo China zikiongonzwa na Shanghai Maglev ambayo inakwenda km 450/h. Nadhani train inayoshika namba 10 au 11 ni ile ya Itally Fresiiarosa, ambayo ina speed ya km 300/h.

Sasa hii ya kwetu (SGR) ambayo inasemekana iatakuwa na speed ya km 160/h haiwezi kuwekwa kwenye daraja moja na hizo train nyingine za wenzetu. Hata Ile train ya Morroco (ONCF AL Boraq), inaspeed ya km 320/h, yaani inatoka mkuku mara mbili ya SGR yetu. Sasa, ni vipi utalinganisha train yetu na za wenzetu?

Tujaribu kutopenda makuu na kujipongeza hapo tulipofikia. Hebu fikiria kidogo, yaani Tanzania tunajenga train yetu wenyewe miaka 120 tangu wajerumani na waingereza watujengee reli ya Kati na ya kaskazini. Hii ni hatua kubwa sana kwa nchi yetu. Tunapenda kulilia vizuri vya wenzetu na kukebehi vya kwetu wakati uwezo hatuna.

Mwenyezimungu awajaalie waasisi wote wa huu mradi (SGR) bila kumsahau shujaa hayati J. P. Maghufuli.
 
Nisiseme mengi lakin hii sio sawa. Ndiyo maana wasomi huwa hawapendwi wala kuaminika wala kueleweka kwa wananchi wa kawaida wengi.

Bora uwe mganga wa jadi kbs tujue moja kuliko hivi.
 
Shida yetu tunaona kama uchumi wetu unaweza kupata kila tunachotamani.Kwa uchumi tulionao bado hatuna uwezo wa kujenga high speed train ndefu labda Moro ingekuwa ndio Dodoma.High speed train ni bei ndefu na ukizingatia tunaimport every thing yaani vifaa hadi watalaam.Lazima uwe na ukwasi wa kutosha.Pia nimegundua watu wanadhani speed inakuwa determined na Train kumbe speed inaanzia kwenye reli yenyewe
 
Hii habari Ina ukweli kiasi gani
Ina maana wametengeneza mafuriko wenyewe kwa bwawa la kuzalisha umeme
 
Mimi huwa siku zote siwaamini wana siasa ni Waongo hata kama angelikuwa ni baba yangu mzazi ni mwana Siasa Nisingelimwamini hata kidogo Walikuw akila siku wanatuambia eti treni ya Mwendo wa kasi kumbe walikuwa wanatuongopea wanatufanya sisi Wananchi kama watoto wa kuwazaa Ahhh kazi kweli iendelee. CCM Oyee Kidumu milele chama SISI EMU......................
 
Mkuu hakuna haja ya kujenga VITU ambavyo vimepitwa na Wakati
Baada ya muda tuje tung'oe Tena hio ni hasara kubwa Sana

Ingekuwa hizo za high speed hazijabuniwa tungekubali kuanza na hizo

Ni Bora tungejenga high speed KUTOKA Moro Hadi Dar
Then tujipange Tena

Hii Dunia inaenda Kasi Sana kwenye tech ,
Hamna muda wa kupoteza na tech ya kizamani
 
Masaa 3 ni Dar to Dom. Dar to Moro ni masaa 1.5. Siyo mbaya sana.
Narudia tena, kwa spidi ya ile treni masaa matatu ni Dar - Morogoro, Dodoma hiyo ndio habari nyingine kabisa.

Prof. Mbarawa muongo.
 
Kuna reli ya mkoloni ambayo bado inatumika, sasa kulikuwa na sababu gani ya kujenga SGR ambayo haitakuwa na treni yenye kasi?

Sambamba na ujenzi wa SGR, hiyo reli ya zamani imekarabatiwa kwa gharama kubwa.

Siasa zetu zina ujinga mwingi sana.
SGR ni mpango wa kishamba wa JPM, bora wangejenga barabara njia 4 mpaka mikoa ya Mwanza,Kigoma Arusha na Mbeya
 
Kaka yake na Samia mtata sana!
Walivyoanza kuingiza vichwa used pale ndiyo nilianza kujua kuwa hii project ni white elephant!
 
au mabasi manake mabus dereva akikaza muda huo yupo dar,nchi ngumu sana hii aiseeee hata hawaogopi wanakula mpk mbegu
 
Wamenunua vichwa vya Hali ya chini,Ili kulinda malori na mabasi yao
 
Kama ulishawahi kupanda hayo ma high speed train na bullet train
Hawa TRC unawaona kama wababaishaji tu

Ova
 
Walishapigwa kamba na Mwendazake 🤣🤣🤣

Sema hivi design ya Sgr inaruhusu Mwendokasi ila hatuna pesa za kununua vile vichwa vya kusukuma huo Mwendokasi ndio maana wamenunua used.
 
Nimemuelewa mdau kuwa ufanisi mdogo,ila bado masaa 3 dom,hata zile vx,8 na korokoro zifananazo na hizo za siiirikali bado haziwezi toboa dom masaa 3😁
halafu pia kuna muda wa kusimama vituoni kushusha na kupakia abiria, hata kama ni dakika kumi kumi. Au likitoka Dar ndiyo kimoja mpaka Moro halafu Dodoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…