Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
😆😆😆😆😆😆
 
Aliyeenda JPM kuanzisha bwawa la mwl Nyerere lilikuwa la kuupa msukumo SGR. Sasa mmekuja na longolongo nyingine.

Majuzi mmewaambia wanaoishi ukanda wa Rufiji na Kilwa eti Wahame kutokana na athari za maji mliyoyafungulia wenyewe ya bwawa .
Kama sio mwanzo wa kuhujumu hili bwawa ni nini!
Mwisho wa siku hakutakuwepo na maji!

Hao wananchi mliowafungulia hayo maji waende wapi na je mko tayari kuwalipa fidia kwa uzembe huo?
WaTanzania msiwafanye wajinga.
Katiba mpya Katiba .
sasa wewe ulitarajia mto rufiji ukitema maji yaende wapi? bwawa lina uwezo wake wa kuhifadhi maji, yanayozidi lazima yaachiwe yaende mbele. Hapo uhujumu uko wapi?

Hizo 'impacts' zilitakiwa ziwe zimetengenezewa mpango wake mapema kabla ya kuanza ujenzi, na pia watu walitakiwa wawe wamehamishwa downstream (yaani iwepo resettlement plan), yote hayo yawe yamefikiriwa utekelezaji wake kabla ya kuanza ujenzi wa hilo bwawa. Umewahi kusikia 'Environmental and Social Impact Assessment' ya mradi?

Ndiyo hayo sasa wacheni kulaumu kila kitu na ati kudai katiba mpya, hiyo katiba mpya itafanya nini?
 
Nimecheka kwa nguvu vibaya sana, treni sio ya mwendokasi, ila gharama za ujenzi ni za treni ya mwendokasi!
Mbongo kupigwa kawaida yetu, mbongo wenzetu atupige,hapo bado mdhungu😁
 
Teh! Wewe ndiye hukuelewa toka mwanzo. Kilichokuwa kinajengwa ni standard gauge railroad (SGR) na sio high speed railroad (HSR) ! Mjifunze ku-read between the lines kauli za wanasiasa.
Sahihi
Kweli ni SGR sio high speed
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
Jamaa wameshapiga pesa wanakuja kivingine
 
Ata ivyo wabongo ndo tunamakosa tunashindwa kutofautisha treni ya umeme na treni ya mwendo kasi
Treni yetu ni treni ya umeme inatumia umeme badala ya mafuta au makaa ya mawe
 
Wabongo wanataka mjusi bado hatujafika level hizo tunaenda taratibu
 
Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.

Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".

Source: ITV habari.

My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?
Mkuu unatembea na IST toka Dar mpaka Dodoma na unafika masaa matatu???
Embu kuwa serious kaka ni 440+km zile.
IST top speed ni 180kmph.
Aya niambie na foleni za road unafikaje kwa masaa matatu???
 
Mbarawa kasema top speed ya treni yake ni 160 kmh. Sasa kama top speed ya IST ni 180 kmph ipi Ina speed zaidi?
Kumbuka reli haikai foleni na hakuna traffic jam.
UNATAKA KUNAMBIA UNAWEZA UKA MAINTAIN SPEED YA IST YA 180KMPH MPK UNAFIKA DODOMA???
Kuwa serious mkuu.
 
Hiyo tofauti ya ujenzi kati ya reli za China na Korea na hii reli yetu ya SGR ni ipi?

Nina wasiwasi Mbarawa asijekutumia udhaifu wao wa kununua vichwa chakavu vya treni ya SGR, vilivyosababisha spidi iwe ndogo, akahamishia kwenye ujenzi wa reli.

Maana naona siku hizi ni kama kuna mchezo huko serikalini wa kumtupia lawama The late Magufuli kwenye kila kitu.

Wajanja wamekula pesa kwenye ununuzi wa vichwa vya treni, wameachwa hawafanywi chochote na bosi wao, wapo tu wanatamba kwa ukwasi..

Leo malengo ya utengenezaji wa reli ya SGR ili kurahisisha usafiri yameshindwa kufikiwa, lawama inatupiwa njia ya treni!.

Mbona hili jambo halikuwahi kusemwa kabla? sasa kuna maana gani ya kuwa na hiyo reli ya SGR?

Prof. Mbarawa ameonesha incompetence muda mrefu sana kwenye hiyo wizara, ajabu anaachwa tu, na haya ndio matokeo yake.

Kwa kauli hii ya Prof. Mbarawa, sasa hata ujenzi wa JNHPP nao hauna maana, lile bwawa sasa limegeuzwa la kutuondolea ile migao yao ya umeme wanayoitengeneza, yale malengo mahususi ya kuzalisha umeme wa kuendesha treni ya SGR yamekufa.

I doubt kama yupo atakayekuwa tayari kupoteza muda wake atoke Dsm kwenda Morogoro kwa masaa matatu, wamechezea pesa nyingi, wamepoteza muda, wameshindwa kufikia malengo.
Hielewi unachokisoma au ni upoyoyo tu?

Kishasema hii yetu siyo treni ya mwendo kasi "not high speed train".

Kuwa na SGR hakumaanishi treni ya mwendo kasi.
 
Kumbuka reli haikai foleni na hakuna traffic jam.
UNATAKA KUNAMBIA UNAWEZA UKA MAINTAIN SPEED YA IST YA 180KMPH MPK UNAFIKA DODOMA???
Kuwa serious mkuu.
Unaanza safari saa 9 usiku barabara ikiwa haina vurugu, by 12 asubuhi ushaiona Chalinze ya Dodoma
 
Mimi huwa siku zote siwaamini wana siasa ni Waongo hata kama angelikuwa ni baba yangu mzazi ni mwana Siasa Nisingelimwamini hata kidogo Walikuw akila siku wanatuambia eti treni ya Mwendo wa kasi kumbe walikuwa wanatuongopea wanatufanya sisi Wananchi kama watoto wa kuwazaa Ahhh kazi kweli iendelee. CCM Oyee Kidumu milele chama SISI EMU......................
Hivi kutoka 40 km/hr Hadi 160 km/hr siyo mwendo kasi?
 
Back
Top Bottom