Prof. Mbarawa: Treni za SGR ni za mwendo wa kawaida (siyo mwendokasi)

Hivi kutoka 40 km/hr Hadi 160 km/hr siyo mwendo kasi?
Natafuta clip ambayo yule rais kichaa alitamka hadharani kuwa treni itatumia masaa 3 kutoka DAR mpk Mwanza. Nikiipata nafungua uzi
 
Masaa 3 mpaka Dodoma inatosha
Amesema si kama za China lakini kwetu sio mbaya.
 
Unaanza safari saa 9 usiku barabara ikiwa haina vurugu, by 12 asubuhi ushaiona Chalinze ya Dodoma
Una amini unaweza maintain hiyo speed mkuu!?
Unaamini kuna usalama kabisa!?
Maana kuanzia pale Chalinze mpaka Mikese kuna road nyembamba sana.
 
Mkuu unatembea na IST toka Dar mpaka Dodoma na unafika masaa matatu???
Embu kuwa serious kaka ni 440+km zile.
IST top speed ni 180kmph.
Aya niambie na foleni za road unafikaje kwa masaa matatu???
Mnatak kufananisha 180kmph ya ist na ya land cruiser mko seriois kwelii[emoji23][emoji23]...50km/h ya sgr inaweza zaidi kua kama 180 ya ist..kwasababu speed ya treni ni uniform...gari inabadilika badilika
 
Mnatak kufananisha 180kmph ya ist na ya land cruiser mko seriois kwelii[emoji23][emoji23]...50km/h ya sgr inaweza zaidi kua kama 180 ya ist..kwasababu speed ya treni ni uniform...gari inabadilika badilika
Ndio mimi namuuliza jamaa kwa IST kweli afike Dodoma kwa masaa matatu???
Hapo bado foleni hapo bado kupoa kwa hilo boksi la usafiri IST.
 
Kadogosa anafanya nini hapo si alipaswa kuwa sehem kama segerea
 
Hivi kutoka 40 km/hr Hadi 160 km/hr siyo mwendo kasi?
Ni mwendo kasi.
Ila kuna mwendo wa haraka zaidi ambao ndio hizo higher speed train zinazotembea hadi 600kmph yani toka Dar mpaka Singida kwa lisaa.
Hii yetu ni standard speed train mkuu.
Hizo higher speed train hutembea katika broad gauge railway na maglev rail tracks.
 
Kumbuka hii treni ina vituo njiani,inatakiwa kushusha na kupakia abiria lakini bado inatumia saa 1.30,sasa ikiamua tu ikimbie bila ya kusimama si itakuwa shida...
 
Bado ni nafuu sana kutumia masaa 3 kwasababu Dar - Dodoma kwa Bus ni masaa 9 kwahiyo kuna unafuu sana
 
Bado ni nafuu sana kutumia masaa 3 kwasababu Dar - Dodoma kwa Bus ni masaa 9 kwahiyo kuna unafuu sana
Siyo kweli mkuu, itakuwa wewe huwa unapanda Toyo. Kutoka DAR mpk Dodoma ni masaa 7 tu
 
Nakubaliana na wewe kabisa, isipokuwa wakati mwingine unajikuna pale unapoweza. Kwa hali ya ya uchumi wa nchi, ambao bado unategemea huruma za wahisani na mikopo, inabidi tupange na kuchagua kipi cha kufanya sasa hivi na kipi kifanywe baadae.

Haiwezekani nchi ijiingize kwenye mega economic development projects zaidi ya sita, ambazo zinagharimu trillion of shillngs, na ambazo tunategemea kukoapa na kupewa na wafadhili, halafu tutegemee kupata World class results. Binafsi, sidhani kama that is possible hata kidogo.
Hebu angalia hii miradi ya maendeleo ambayo nchi iliamua kuianzisha kwa ajili ya maendeleo ya nchi:
-SGR
-Mwalimu Nyerere Hydro Electric Dam
-Daraja la Busisi/ Kigongo
- Tanzania/ Uganda pipeline kutoka Tanga
-Kuna miradi kibao ya mwendo kasi inaendela hapo Bandari Salam.
-Kuna lile daraja kule kwa matajiri, Msasani Peninsula
- Nasikia Kuna project nyinge ya kutandaza Cable wire kule Mt. Kilimanjaro kwa ajili ya utilii.

Hii yote ni miradi mikubwa sana Na yenye gharama. Bila kuweka kipaumbele, kuna baadhi ya miradi tutabambikiwa tu au itakamilishwa below standard. Kuna msemo kwenye lugha ya wakoloni , unasema, "Don't bite off more than you can chew". Na ndicho tunachofanya.

Binafsi naona ni vizuri turidhike na kile tunachoweza kumudu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…