Prof Mchembe: Wanaoruhusiwa kutoa taarifa za Afya ni Waganga wa Mikoa na Wilaya siyo Wanasiasa

Kumbe fukuto la Waziri wa Afya kumtimua Daktari wa Wliaya Chunya limechukua sura nyingine...
Na Chalamila nae amekuwa msemaji wa wizara kule Mbeya.

Bado naona majaribio ya uongozi kwenye hii awamu ya tano tena.

Juzi Dmo huko Mbeya katoa taarifa ya mlipuko waziri kapaa nae.

Leo Katibu mkuu anasema Dmo ana mamlaka ya kutoa taarifa za wilaya yake.

JPM alifanya makosa makubwa sana kuweka safu isiyo na uzoefu. Wachumia tumbo.

Hebu ona Lukuvi na Mkuchika wanavyo toa maamuzi yao kwa busara..
 
Kadhalika Prof Mchembe amesema Corona ni ugonjwa wa mlipuko wa maambukizi kwa njia ya hewa kama ilivyo chorela kwa mfumo wa chakula.

Source ITV habari
Sasa kwanini huwa tunakuwa serious kwenye response ya Cholera (emergency operation centers, vituo vya karantini, daily data updates kutoka kila wilaya etc) ila kwenye corona tunasema haipo ipo haipo?

Prof. Mchembe kuna kitu anatamani kusema/kufanya ila uongozi wa Nchi bila shaka haupo tayari
 
Labda!
 
Sasa hao RMO au DMO wathubutu kutoa taarifa ya corona; hapo ndipo utakapoona vurugu 'match'.

Hivi huyo Katibu Mkuu wa Afya ni Profesa wa vitu gani?
Naona anajichanganya sana. Naye kaokotwa "Jalalani"?
 
serikali inapenda kusifiwa tu, huku ikificha aibu zake. Angalia walivyoumbuka Angola, wanapeleka Corona huko, wanazuiwa airport kwamba rudisheni ujinga wenu kwenu.
 
'MIGNON', huwa nakusoma, lakini sijawahi kukusoma hivi! GT.
 
Profesa hana muda wa kujibu maswali kama haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…