Prof. Mkenda akabidhi Vitabu vya Kidato cha Sita vya Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK), aipa kongole TET

Prof. Mkenda akabidhi Vitabu vya Kidato cha Sita vya Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK), aipa kongole TET

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-07-22 at 23.14.35.jpeg
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tkenolojia, Prof. Adolf Mkenda amekabidhi Vitabu vya Dini ya Kiislamu (EDK) kidato cha Sita kwa Baraza Kuu la Waisalam wa Tanzania (BAKWATA), Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar huku akipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kufanikisha Vitabu hivyo.

Waziri Prof. Mkenda amekabidhi Vitabu hivyo 22/7/2026 katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mfalme Muhhamed wa Sita (Bakwata Makao makuu), na kuudhuriwa na wadau mbalimbali wa dini ya Kiislamu, wakiwemo viongozi wa dini na Serikali.

Awali, Waziri Prof. Mkenda amesema: Serikali itaendelea kutekeleza Sera ya Elimu katika kuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata elimu iliyo sawa na yenye ubora.

Ameishukuru BAKWATA kwa kuweza kusaidia mchakato wa kuwezesha Vitabu hivyo kwani kupitia Mufti Mkuu, waliweza pia kuanzisha mpango wa taasisi ya kusimamia ufundishaji wa dini ya Kiislamu shuleni (TISTA).

"Mchakato huu umefanywa kwa karibu sana na Waisalam wote, kama tulivyopata Baraka ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, lakini pia Mufti Mkuu na wadau wote wa dini ya Kiislamu.

Kupitia TISTA chini ya BWAKATA hakuna Mwanafunzi atakayekosa elimu yenye ubora.

“Kila mwanafunzi nchini atapata elimu kwa ubora kama wanafunzi wengine na leo hii tumekabidhi vitabu vya elimu ya dini kwa wanafunzi wa kidato cha sita nina imani kuwa vitatumika sawa sawa na ilivyokusudiwa.

Katika maboresho ya Sera ya Elimu na Mitaala yaliyofanyika mwaka 2023, maoni mbali mbali ya kuanzishwa kwa somo la elimu ya dini ya Kiisilamu yalitolewa na wadau mbalimbali na baadae kuwezeshwa kwa mchakato wa uandishi wa vitabu hivyo vilivyokabidhiwa kwa TISTA kupitia Baraza la Waisilamu nchini (BWAKWATA).

Prof. Mkenda, ameishukuru TET kupitia Mkurugenzi Mkuu, Dkt.Aneth Komba kwa kuhakikisha kuwa uandishi na uchapaji wa vitabu wa vitabu unamalizika kwa haraka jambo ambalo litasaidia wanafunzi kuanza kuvitumia shueleni.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISTA, Bw. Musa Kundecha ameshukuru kwa upatikanaji wa vitabu amabvyo ameeleza kuwa ni hatua nzuri katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la dini ya Kiisilamu.

Naye mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Naibu Kadhi, Bw. Ali Ngeruko amesema kuwa ni hatua muhimu katika elimu ya wanafunzi katika dini nakuwa italeta chachu ya kuendelea kujifunza zaidi huku akiishukuru Serikali kwa jitahada za uletaji wa vitabu kama ilivyoahidi.

Vitabu hivyo vitagawiwa katika shule zote Tanzania Bara na Visiwani ambapo wanafunzi wanaosoma somo hilo wataweza kufikiwa.
 
Honestly elimu ya dini inasaidia nini kwa watoto wetu.
Miskiti na makanisa yameona haitoshi.kufundisha sundays na madrasa sasa mnawapelekea watoto.delusions zenu zisizo na maana yoyote ?
 
Ni ujinga na upuuzi mtupu, inasaidia nini hiyo dini? Watu wanataka kuunda vitu nyie mnaenda kugawa vitabu vya kijinga. Mko serious au mnafanya siasa za kipumbavu? Dini hiyo inaleta ugunduzi gani? Ujinga mtupu mnarisha watoto, shame on them. Watu tunataka vitabu vya sayansi na teknolojia, msituletee hadithi za mtume na allah, hizo abrakadabra wanaozitaka waende misikitini wakadanganyane na kupumbazana huko
 
Kwakweli nchi kuja kupata maendeleo sio leo
 
Ni bora tungeomba vitabu vya wachina tuvisome tujue kutengeneza vifaa na zana mbalimbali za kurahisishha kazi zetu, kuzalisha kwa wingi bidhaa zetu, kuzalisha kwa wingi mazao yetu shambani. Sasa vitabu vya dini ya kiislam vina tija na faida gani kwa watanzania wa sasa kama si kudumaza akili za watoto wa taifa hili?
 
...... ndivyo inavyotakiwa, wengine wachungaji, wengine mashehe wasomi na wengine tugombee ajira na kilimo!
ITASAIDIA MGAWANYO WA MAJUKUMU!
 
Pale watu wanapoingia kwenye zama za AI alafu kuna mt anawarudisha nyuma kwenye enzi bibilia na koroani
 
Hivi hawakutokea wasomi/watunga sera wa kupinga ujinga huu kwenye mitaala?
 
Sidhani kama huyu profesa alichokifanya ni utashi wake, maandiko ya kuruani yanasaidia nini kama si kuzidisha kupumbaza watu? Atakuwa anaridhisha waislam ili waone dini imo kwenye mtaala wa taifa.
 
Sidhani kama huyu profesa alichokifanya ni utashi wake, maandiko ya kuruani yanasaidia nini kama si kuzidisha kupumbaza watu? Atakuwa anaridhisha waislam ili waone dini imo kwenye mtaala wa taifa.
Hivi angagawa bibilia; agalo la kale na jipya ungetoa povu kiasi hicho?
 
Hivi angagawa bibilia; agalo la kale na jipya ungetoa povu kiasi hicho?
zipo taasisi za kugawa bibli mashuleni na vyuoni, tena hugawiwa kwa wote bila ubaguzi. Huwajui Wagideoni? Wakristo wapo upstair na imani yao, si watu wa kujioneshaonesha kinafiki, kwanza wana elimu kubwa ya ulimwengu huu
 
Sawasawa!
 
Nadhani mambo ya dini yangeachwa kwenye taasisi zao za kidini ukitambua hii nchi haina dini.
 
Back
Top Bottom