Prof. Mkenda akiri msingi dhaifu wa Kiingereza chanzo cha wengi kufeli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekiri kuwa msingi dhaifu wa mafunzo ya lugha ya Kiingereza kwa wanafunzi wa sekondari nchini umechangia kwa kiasi kikubwa matokeo mabaya ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2024.
 
Naona wastani wa F kwenye English ni 25% ila wastani kwenye Mathematics(Hisabati) walopata F ni 81.5%

Kuna tatizo kubwa tena zito sana kwenye Maths kuliko hiyo kingereza(Hesabu haichagui Lugha) Ila iko hivyo
 
naskia kuanzia form 3 wa mwaka huu hakuna kukimbia physics hatakama unachukua business

mbona watasema, phy hesabu, math hesabu
 
Naona wastani wa F kwenye English ni 25% ila wastani kwenye Mathematics(Hisabati) walopata F ni 81.5%

Kuna tatizo kubwa tena zito sana kwenye Maths kuliko hiyo kingereza(Hesabu haichagui Lugha) Ila iko hivyo
Sasa kama mathe ni ngumu, kuisoma kwa kiingereza si ndo hatari zaidi
 
Hapana Bado Physics ni Option .. Na pia form 1 mwaka huu ana chagua akiwa kidato cha kwanza na sio kidato cha tatu... Ina maana mtoto anaamua achukue physics au aache akiwa form 1
 
Naona wastani wa F kwenye English ni 25% ila wastani kwenye Mathematics(Hisabati) walopata F ni 81.5%

Kuna tatizo kubwa tena zito sana kwenye Maths kuliko hiyo kingereza(Hesabu haichagui Lugha) Ila iko hivyo
Mimi nadhani msingi mzima wa Elimu ya Tanzania ni mbovu wala sio Kiingereza pekee, ukijaribu kufuatilia Elimu yetu haimwandai mtu kuweza kujitegemea pasipo kufikiria ajira Serikalini
 
Kama walimu wenyewe tu hawako competence kwenye kiingereza watafundisha nini? Kituko zaidi kiko kwenye shule za english medium utacheka uzimie! Wanafunzi wanaongea kiingereza kibovu walichofundishwa na walimu wao incompetence. Shule inaitwa english medium lakini lugha ya kiingereza ni shughuli pevu
 
Hapana Bado Physics ni Option .. Na pia form 1 mwaka huu ana chagua akiwa kidato cha kwanza na sio kidato cha tatu... Ina maana mtoto anaamua achukue physics au aache akiwa form 1
....kulingana na ufaulu wa Darasa la Saba..
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekiri kuwa msingi dhaifu wa mafunzo ya lugha ya Kiingereza kwa wanafunzi wa sekondari nchini umechangia kwa kiasi kikubwa matokeo mabaya ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2024.
View attachment 3195497
Walimu wa kiingereza na hisabati wapo wengi mtaani, wapeni ajira basi wasaidie kutatua tatizo
 
Kama walimu wenyewe tu hawako copetence kwenye kiingereza watafundisha nini? Kituko zaidi kiko kwenye shule za english medium utacheka uzimie! Wanafunzi wanaongea kiingereza kibovu walichofundishwa na walimu wao incopetence. Shule inaitwa english medium lakini lugha ya kiingereza ni shughuli pevu
Hata waziri mwenyewe sio competent kwenye hiyo lugha.
 
....kulingana na ufaulu wa Darasa la Saba..
Hapa ndo sehem walipo feli... Kwasabahu la saba kuna Science ambayo mtoto hajuai Physcis ni nn Au chemistry au History.

Yaan History Biology Physics na Chemistry yamekuwa masomo mtoto atachagua akiwa form 1.. hofu yangu ni kuwa hajui anachikichagua kikoje .. angesoma hata mwaka mmoja aone muelekee hapo sawa
 
Ningeulizwa mimi ningesema, kinachofelisha wanafunzi ni kukosa msingi wa HESABU. Mwanafunzi ambaye hajui hesabu hawezi kufaulu, Hesabu, Physics na Chemistry, Book keeping, commerce nk
Kwa ujumla, changamoto ya Elimu yetu ina anzia kwenye kukosa msingi wa HESABU, wala tusilaumu mtu...
Naomba atuletee na waliopata sifuri za hesabu....
Wale walikutana sekondari na wanafunzi waliotokea English medium watanielewa kuwa Hesabu ndio engine
 
Naona wastani wa F kwenye English ni 25% ila wastani kwenye Mathematics(Hisabati) walopata F ni 81.5%

Kuna tatizo kubwa tena zito sana kwenye Maths kuliko hiyo kingereza(Hesabu haichagui Lugha) Ila iko hivyo
Wabongo wavivu wakufikiri na namba zataka ukune kichwa kweli kweli
 
Back
Top Bottom