Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Licha ya kutofafanua ttizo hilo, Waziri amesema tayari Elimu ya Awali, Darasa la Kwanza na la Tatu wanaendelea na Mtaala mpya, Darasa la Pili wanaendelea na Mtaala wa Zamani, Wanaosomea Ualimu pia wanasomea Mtaala mpya.
Akizungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda amesema kuwa wizara ipo katika mchakato wa kuunganisha mifumo ya elimu iweze kuongea kwa pamoja
Waziri huyo ameongeza kuwa lengo ni kuona mifumo hiyo inawezesha kumfuatilia mwanafunzi kuanzia anapoanza elimu ya awali mpaka anapofika elimu ya juu na hata kama atakuwa amekwenda katika mfumo mwingine wa elimu ambapo kwa sasa ni ngumu kufata taarifa sahihi za wanafunzi katika ngazi mbalimbali.
"Kwa kweli kuna umuhimu wa kuwa na mifumo inayosomana na kuzungumza pamoja hii itatuwezesha kupata takwimu sahihi za wanafunzi ili tujue walipo wanafunzi hata kama watakwenda kwenye mfumo wa Cambridge," amesema Waziri
Aidha, Prof. Mkenda amesema ni Muhimu kwa Vyuo Vikuu vinavyojenga kampasi mpya katika mikoa mbalimbali kuwa na programu za kutoa shahada za amali badala ya kutoa taaluma ambazo tayari zipo katika vyuo hivyo.