Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo, Februari 1, 2023 kwenye Mkutano wa 10, Kikao cha 2
RATIBA YA LEO
Kuhusu uamzi wa NECTA kutokutangaza orodha ya Shule 10 bora pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, Mbunge Mwita Getere ameomba mwongozo akiitaka Serikali kuondoa sintofahamu kubwa iliyopo mtaani.
Akitoa majibu ya Serikali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ilikuwa ni kawaida tangu miaka ya 1990, baraza lilikuwa likitoa orodha ya inayoonesha shule gani imefanya vizuri zaidi kwenye mtihani, baadae kwenye Big results now kukawa na mkakati wa kupima ubora na ufanisi wa shule kwa kuangalia wanafunzi wamefaulu vipi kwa kuangalia mtihani wa mwisho wa darasa la saba, form 4, form 6 pamoja na kutangaza shule zipi zimefanya vizuri na zipi zimefanya vibaya, halmashauri ipi imefanya vizuri na ipi imefanya vibaya pamoja na kulinganisha mikoa iliyofanya vizuri na ile iliyofanya vibaya.
Kigezo ilikuwa ni kuangalia matokeo ya mwisho.
Mwezi Novemba, kupitia kikao chake, Baraza liliamua kuacha kuchukua jukumu lenyewe kutangaza ni shule ipi bora kwa kutumia tu matokeo ya mwisho ya mtihani.
Kwahiyo, matokeo ya mwisho ya darasa la saba yaliyotangazwa Disemba 1, 2022, Baraza halikutangaza shule 10 bora au shule 10 za mwisho. Kadharika, matokeo yaliyotoka juzi ya form 4, baraza halikutangaza ni shule zipi bora na zipi za mwisho.
Hata hivyo, takwimu zote zinazohusu kutangaza shule gani imepata A nyingi zaidi, ipi imepata kidogo, ipi ya mwisho zipo hadharani, siyo siri. Isipokuwa baraza limejiondolea jukumu la kusema ni shule ipi bora. Takwimu hazijafichwa, mtu mwingine yeyote anaweza kuzitafuta na kuzipata.
Akifafanua zaidi kwanini Baraza limejivua jukumu hilo la kutangaza, Waziri ametoa sababu zifuatazo-
RATIBA YA LEO
- Dua
- Hati za kuwasilisha mezani
- Taarifa za kamati
- Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii
- Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira

- Utata uliopo kwenye kutathimini shule bora kutokana na kutokuwepo kwa usawa wa idadi ya wanafunzi kwa kila shule.
- Utaratibu wa kutangaza shule hizo ulikuwa unazingatia matokeo ya mwisho pekee pasipo kuangalia mchango wa shule kwenye matokeo ya mtoto husika. Njia hii hujulikana kama raw scores imeacha kutumika kwenye nchi nyingi duniani.
- Kuna njia zingine mbili ambazo ni kutathimini mchango wa shule kwenye kuongeza ubora wawanafunzi (Value addition) na Kutambua utofauti wa mazingira ya wanafunzi (contextual value addition approach), hivyo ikiwa kwa baadae zitafanyiwa kazi zinaweza kutumika katika kutangaza matokeo ya shule kama ilivyokuwa zamani.