amadala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2017
- 4,265
- 12,268
Wizara ya elimu chini ya Profesa Mkenda hii aibu mnaitaka bila sababu. Kama mlijua fedha hakuna kulikuwa na haja gani ya kuita waalimu toka mikoani kuja Arusha kwenye semina na wamekaa wiki mbili mpaka wanamaliza tarehe 2 Mei,2023 hamjawalipa fedha zao.
Huu mradi wa SEQUIP imefadhiliwa na benki ya dunia na una hela za kutosha. Kwa nini waalimu zaidi ya 250 toka mikoa 12 mnashindwa kuwalipa baada ya semina na sasa wanalalamika hivi?
Hivi kwa nini mnapenda kudharau waalimu? Haya mambo mngefanyiwa bungeni mngeelewa? Mnaposema mfumo wa kulipa fedha huko hazina unasumbua hilo linawahusu vipi waalimu mliowaita kuja kwenye hii semina? Kama mlikuwa hamjajipanga kulikuwa na haja gani kuwaita kuja kufanya semina?
Kuna muda huu utendaji wenu mbovu ndiyo chanzo cha watu kuichukia serikali kwa sababu hamjali mambo ya watu wengine na mnaona wanastahiki kupata shida.
Profesa Mkenda hili jambo ni la hovyo sana kiutendaji na unatakiwa kuheshimu waalimu hawa na kuchukua hatua haraka sana. Walipeni fedha zao na msirudie tena kuandaa hizi semina kama hela hakuna.m kuliko kutesa Hawa walimu kiasi hiki.