Prof. Mkenda: Waziri hana mamlaka ya kuingilia chuo kama umefukuzwa kwa kudanganya

Prof. Mkenda: Waziri hana mamlaka ya kuingilia chuo kama umefukuzwa kwa kudanganya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Snapinsta.app_450508498_838739731653431_4541002653020168925_n_1080.jpg
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kama Waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini hatoingilia mamlaka za Vyuo Vikuu zinapochukua hatua mbalimbalu za kinidhamu katika udanganyifu wa mitihani

Kauli hiyo ameitoa Julai 12, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari juu ya udanganyifu katika vyuo vikuu hasa kwenye masuala ya mitihani ambapo amesisitiza kuwa katika vyuo vikuu mtu akifanya udanganyafu katika mtihani adhabu ni kufukuzwa chuo.

‘’Kila tunaposikia tuhuma tunachukulia kama jambo zito sana, kulikuwa na dalili kama hizo katika mitihani ya darasa la saba, kidato cha Nne na Sita, na tulichukua hatua kali, ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata maslahi ya baadhi ya wawekezaji katika sekta ya elimu’’ Alisema Mkenda.

Ameongeza kuwa suala la udanganyifu katika mitihani lina madhara makubwa kwani linaondoa usawa, na kwamba Serikali inataka Wanafunzi wanapofanya mitihani wapimwe kwa usawa na haki, isitokee mmoja anafanya mtihani kwa udanganyifu na kufaulu wakati mwingine anatumia juhudi zake.
Snapinsta.app_450662614_1137321520690541_7882615460853831450_n_1080.jpg

Snapinsta.app_450102852_1025475501834207_3704847237397967381_n_1080.jpg

Snapinsta.app_450495743_356730377528219_2306844129501254576_n_1080.jpg
 
Elimu ya Tanzania ni shida tu sielewi ata kazi ya TCU ni nini Vyuoni
 
Back
Top Bottom