Prof. Mohamed Janabi Miongoni mwa Wagombea wa Ukurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
PROFESA Mohamed Janabi, jina lake limetangazwa rasmi kuwa miongoni mwa wagombea watano katika kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ajaye wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Kanda ya Afrika.

Prof. Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anawania kiti hicho pamoja na wenzake miongoni mwao kutoka nchi za Afrika Magharibi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, limetoa taarifa hiyo. Majina ya wagombea hao ambayo yatafanyiwa mchakato wa Uchaguzi Mei 18, mwaka huu, yaliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Soma Pia: Rais Samia ampendekeza Profesa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO-Afrika

Nchi wanachama yaliwasilishwa majina hayo kwa kiongozi huyo, leo, Machi 14, 2025 huku nchi tano ikiwamo Tanzania na nyingine nne Ivory Coast; Togo; Niger na Guinea pia wakifanya hivyo.

Wagombea kutoka nchi zingine ni Dk. N'da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast; Dk. Dramé Mohammed Lamine (Guinea); Dk. Boureim Hama Sambo (Niger); na Pr Mijiyawa Moustafa wa Togo.
 
Ivory coast wachukue hilo kombe.
 
Tunashauri wagombea wote wa nafasi hizi,Moja ya kigezo cha kufanya interview,kiwe, mgombea kupimwa afya yake na wapimwe na wataalam wa WHO.
 
Marehemu alikuwa na sifa tofauti na huyu!
Kitakachomponza huyu ni affiliation yake na Watawala! Ukiangalia comments, Marehemu alipokelewa na watanzania Kwa ujumla wake sababu alikua na integrity ya kipekee! Hilo halina ubishi hata kidogo!
Sioni Lucas akimpigia kampeni sijajua kwanini mana anawajua watu wote sifa na sifu wao. Sioni Akienda kushinda kama na Mama Jenista ataemda pia kumnandi, akanza na on behalf of myself
 
Anaandika Zanzibar-ASP :-
Mara baada ya Rais Samia kutangaza kumpigia debe Professor Janabi ili kuiwakilisha Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha ukurugenzi mkuu wa WHO kanda ya Afrika, watu wenye akili kubwa ikabidi waingie chimbo kufukua file lenye kubeba wasifu mbali mbali kumhusu Profesa Mohamed Janabi ili kuona ana kipi cha kielimu na kisayansi, na sasa imekuja kugundulika kuwa, kumbe mwamba hakuwahi kusomea udaktari bingwa wowote (Mmed) achilia mbali udaktari bingwa wa moyo (Cardiologist) na wala hana sifa zozote stahiki za kibingwa kutibu moyo.

Na kwa mifumo ya mamlaka za usimamizi wa fani ya utabibu hapa Tanzania (Medical Council of Tanganyika), daktari asiyekuwa na sifa za kibingwa za fani huzika haruhusiwi kutoa matibabu ya kibingwa moja kwa moja kwa mgonjwa, na kwa tafsiri ya moja kwa moja, Professor Janabi hakuwahi popote moja kwa moja kutibu kibingwa moyo, na kama aliwahi kufanya hivyo anastahili kushtakiwa kwenye baraza la madaktari kwa kutenda kosa la kimaadili katika fani ya udaktari.

Hapa chini nimeambanisha wasifu wa Professor Janabi wa kidaktari unaotambulika na mamlaka za usimamizi wa taaluma ya udaktari hapa Tanzania (MCT).

Mwisho kabisa, MCT wanatakiwa kutoa maelezo kwa umma, kwa hicho ulichowahi kusomea Professor Jababi (Masters of tropical health) ambacho hakina sifa yoyote ya udaktari bingwa wa moyo (maana mhitimu yoyote wa fani ya afya anaweza kusomea), kinampaje sifa mhusika kuwa daktari bingwa wa moyo?

NOTE:
Daktari bingwa mbombezi (kama daktari bingwa wa moyo) yoyote mwenye sifa stahiki za kutambulika na baraza la madaktari la Tanganyika (MCT) ni lazima utambulisho wake kwenye ukurasa rasmi wa MCT (Professional Profile status) usomeke SUPER SPECIALIST DOCTOR. Kwa Professor Janabi hakuna hicho kitu.

Cc imhotep , bagamoyo, DR Mambo Jambo
 
Attachments

  • Snapinsta.app_483423170_1071770781641908_3545649834984004154_n_1080.jpg
    Snapinsta.app_483423170_1071770781641908_3545649834984004154_n_1080.jpg
    126.7 KB · Views: 1
PROFESA Mohamed Janabi, jina lake limetangazwa rasmi kuwa miongoni mwa wagombea watano katika kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ajaye wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Kanda ya Afrika.

Prof. Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anawania kiti hicho pamoja na wenzake miongoni mwao kutoka nchi za Afrika Magharibi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, limetoa taarifa hiyo. Majina ya wagombea hao ambayo yatafanyiwa mchakato wa Uchaguzi Mei 18, mwaka huu, yaliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Soma Pia: Rais Samia ampendekeza Profesa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO-Afrika

Nchi wanachama yaliwasilishwa majina hayo kwa kiongozi huyo, leo, Machi 14, 2025 huku nchi tano ikiwamo Tanzania na nyingine nne Ivory Coast; Togo; Niger na Guinea pia wakifanya hivyo.

Wagombea kutoka nchi zingine ni Dk. N'da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast; Dk. Dramé Mohammed Lamine (Guinea); Dk. Boureim Hama Sambo (Niger); na Pr Mijiyawa Moustafa wa Togo.
Wampe, sio tu kwa Heshima ya Marehemu Dr. Ndungulile, bali pia anaweza sana, na ni mtendaji halisi sio politician.
 
Kila la kheri pro. Janabi! ukishinda watanzania wote Tumeshinda, Nenda katuheshimishe Watanzania, Bi idhini Llah tunaenda kuibuka kidedea.
 
Back
Top Bottom