Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
PROFESA Mohamed Janabi, jina lake limetangazwa rasmi kuwa miongoni mwa wagombea watano katika kuwania nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ajaye wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa Kanda ya Afrika.
Prof. Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anawania kiti hicho pamoja na wenzake miongoni mwao kutoka nchi za Afrika Magharibi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, limetoa taarifa hiyo. Majina ya wagombea hao ambayo yatafanyiwa mchakato wa Uchaguzi Mei 18, mwaka huu, yaliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Soma Pia: Rais Samia ampendekeza Profesa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO-Afrika
Nchi wanachama yaliwasilishwa majina hayo kwa kiongozi huyo, leo, Machi 14, 2025 huku nchi tano ikiwamo Tanzania na nyingine nne Ivory Coast; Togo; Niger na Guinea pia wakifanya hivyo.
Wagombea kutoka nchi zingine ni Dk. N'da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast; Dk. Dramé Mohammed Lamine (Guinea); Dk. Boureim Hama Sambo (Niger); na Pr Mijiyawa Moustafa wa Togo.