Anaandika
Zanzibar-ASP :-
Mara baada ya Rais Samia kutangaza kumpigia debe Professor Janabi ili kuiwakilisha Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha ukurugenzi mkuu wa WHO kanda ya Afrika, watu wenye akili kubwa ikabidi waingie chimbo kufukua file lenye kubeba wasifu mbali mbali kumhusu Profesa Mohamed Janabi ili kuona ana kipi cha kielimu na kisayansi, na sasa imekuja kugundulika kuwa, kumbe mwamba hakuwahi kusomea udaktari bingwa wowote (Mmed) achilia mbali udaktari bingwa wa moyo (Cardiologist) na wala hana sifa zozote stahiki za kibingwa kutibu moyo.
Na kwa mifumo ya mamlaka za usimamizi wa fani ya utabibu hapa Tanzania (Medical Council of Tanganyika), daktari asiyekuwa na sifa za kibingwa za fani huzika haruhusiwi kutoa matibabu ya kibingwa moja kwa moja kwa mgonjwa, na kwa tafsiri ya moja kwa moja, Professor Janabi hakuwahi popote moja kwa moja kutibu kibingwa moyo, na kama aliwahi kufanya hivyo anastahili kushtakiwa kwenye baraza la madaktari kwa kutenda kosa la kimaadili katika fani ya udaktari.
Hapa chini nimeambanisha wasifu wa Professor Janabi wa kidaktari unaotambulika na mamlaka za usimamizi wa taaluma ya udaktari hapa Tanzania (MCT).
Mwisho kabisa, MCT wanatakiwa kutoa maelezo kwa umma, kwa hicho ulichowahi kusomea Professor Jababi (Masters of tropical health) ambacho hakina sifa yoyote ya udaktari bingwa wa moyo (maana mhitimu yoyote wa fani ya afya anaweza kusomea), kinampaje sifa mhusika kuwa daktari bingwa wa moyo?
NOTE:
Daktari bingwa mbombezi (kama daktari bingwa wa moyo) yoyote mwenye sifa stahiki za kutambulika na baraza la madaktari la Tanganyika (MCT) ni lazima utambulisho wake kwenye ukurasa rasmi wa MCT (Professional Profile status) usomeke SUPER SPECIALIST DOCTOR. Kwa Professor Janabi hakuna hicho kitu.
Cc
imhotep ,
bagamoyo,
DR Mambo Jambo