LGE2024 Prof. Muhongo Amejiandikisha Kupiga Kura Tarehe 27.11.2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301


Leo, Ijumaa, 11.10.2024, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amejiandikisha kupiga kura tarehe 27.11.2024.

Vilevile, ametembelea vitongoji kadhaa vya Kata nne, ikiwemo Kata ya kwao ya Kiriba, yenye vijiji 3 na vitongoji 24, na kupata yafuatayo:

(i) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ndani ya Kata ya Kiriba kwa siku ya leo: 1,856.

(ii) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye Kitongoji cha Miembeni (Kituo cha Afya), Kijiji cha Bwai Kwitururu Kufikia saa 6 mchana: 22; Kufikia saa 12 jioni: 50; Prof Sospeter Muhongo amejiandikisha hapo

Uhamasishaji:
Wananchi waendelee kuhamasishwa kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27.11.2024

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, akijiandikisha kupiga kura, na kutembelea vituo kadhaa vya uandikishaji wapiga kura ndani ya kata nne za Musoma Vijijini.

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-11 at 22.13.00(1).jpeg
    58 KB · Views: 3
Profesa mwenye akili aliyezaliwa kwenye nchi ya wajinga.

Sijui tumerogwa na nani nchi hii?? Yaani tunamuweka benchi prof kama huyu halafu tunampa uwaziri wa nishati mwalimu wa primary, Biteko??
 
Profesa mwenye akili aliyezaliwa kwenye nchi ya wajinga.

Sijui tumerogwa na ni nchi hii?? Yaani tunamuweka benchi prof kama huyu halafu tunampa uwaziri wa nishati mwalimu wa primary, Biteko??
Uyu ndie yule wakumuita Kafulila two2?
 
Profesa mwenye akili aliyezaliwa kwenye nchi ya wajinga.

Sijui tumerogwa na ni nchi hii?? Yaani tunamuweka benchi prof kama huyu halafu tunampa uwaziri wa nishati mwalimu wa primary, Biteko??
Huyo Prof hapelekeshwi na wanasiasa wala kujipendekeza.
 
Reactions: G4N
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…