Hii argument nimeisikia na bado nazidi kuisikia, kwamba wasomi wanalazimika kuingia kweye siasa kisa kwenye siasa kunalipa sana kuliko kwenye academics. Mi nina majibu mawili kuhusu hiyo argument. Kwanza nchi yoyote ile isiyoweza kutambua academics wake bora na ikaweza kuwaheshimu na kuwalipa inavyostahili hiyo nchi itabaki kuwa duni sana. Pili kuna shida kwa wasomi wetu ambao hawawezi kuwa proud na taaluma zao na wakajifanya cheap kwa kujiuza kwingineko wasikostahili eti kisa kunalipa. I can understand msomi ngazi ya profesa kuwa advisor wa serikali kwenye mambo yanayohitaji utaalamu. Lakini profesa kabisa, mtu aliyespend zaidi ya nusu karne akispecialize kwenye kitu kimoja flani afu anaacha kabisa taaluma yake na kwenda kugombea ubunge? Hapo kuna shida. Pia ni tabia mbovu kabisa kwa watawala wetu kuwateua maprofesa kwenda kufanya kazi trivial za adminstration kwenye serikali. You dont spend miaka kibao kubobea kitu fulani afu umfanye mtu huyo awe karani wa kusoma mafaili hata kama utamlipa mamilioni ya mshahara na posho. Huku kutoallocate resources appropriately, zikiwemo human na financial resources, kutaitesa hii nchi miak mingi ijayo. Tuna majitu mengi sana yanafanya kazi pasipostahili na tuna watu wengi sana wanalipwa isivyostahili.