Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,272
- 1,120
Wanajamvi nawasalim sana!
Licha na kutingwa na majukumu yangu ya hapa na pale naomba nitumie muda huu kumuomba makamu mkuu wa chuo kikuu (mother of all universities) udsm kuzui rushwa hii. Prof. Wangu natambua anakabiliwa na majukumu ya kuhakikisha taaluma za vijana wetu zinatolewa kwa ufanisi mkubwa sana hivyo kukifanya chuo kubaki kwenye rank za juu kitaaluma. Majukumu haya hayapishani na yale ya kisiasa na kule synovate!
Mkono wangu naunyoosha pale dispensary ya chuo. Sote tumeona vijana wetu wakijiunga na chuo siku hizi chache toka vyuo mbalimbali. Kwa mlimani (sina hakika na kwingine) kuna utamaduni wakuanzisha miradi baada ya first year kujiunga. Miradi hii imekuwa ya kukusanya fedha toka kwa vijana hawa bila mpangalio. Kutokuwa na mpangilio na utaratibu wakueleka mdudu rushwa na ufisadi wa hali ya juu anazidi kuwatafuna watoto wetu.
Pamekuwa na tozo ya Tsh 5,000/- kwa kila mwanafunzi anayetaka kujaziwa fomu ya matibabu. Fomu hii imekuwa ni moja ya kigezo muhimu kuweza kufanikisha zoezi zima la admission kwa mwanafunzi. Well, binafsi sipingi uwepo wa form. Ninachokipinga hapa ni mchakato mzima wa ujazwaji wa form hizo unaoambatana na mikono mochafu ya rushwa. Nilifanikiwa kufika dispensary hapo siku za karibuni kuweza kuangalia zoezi hilo. Nilichogund ua na kuthibitishiwa na wahusika (wanafunzi) ni kwamba huwa wanalipa kiasi hicho cha 5000 bila hata yakufanyiwa vipimo!
Nasema sipingi pia ulipwaji wa fedha hizo. Ninachopinga hapa ni ujazwaji wa form hizo pasi na kufanyiwa vipimo husika. Je lengo hasa la form hizo ni lipi? Hasa ikizingatiwa vijana hao hawapimwi?! Zoezi hili hata sisi lilitukumba nakulipa pesa hizo enzi tunajiunga na chuo. Inakera sana Prof. Naomba ulivalie njuga na ikibidi fanya uchunguzi kubaini tuhuma hizi. Zoezi hili limekuwa likiwaandaa vijana wetu kuwa watoa na wapokea rushwa mapema kabla hawajaanza hata masomo. Na wamalizapo vyuo ndiyo wanafikia kutufikisha kwenye Richmond na mikataba ya kipuuzi ya gas inayoendelea sasa.
USHAURI:
Prof. Rwekaza Mukandala, form hizo zitotelewe na zijazwe bure na madaktari wa hapo chuo. Ikumbukwe kuwa si kila mtu ana uwezo wakulipa hiyo 5000. Tumia wataalamu na taaluma yako kubaini wale wote wanaohusika na mradi huu na wawajibishwe. Ama pawekwe utaratibu mahususi utakaothibisha mtu amapimwa na amelipia (endapo italazimu iwe hivyo). Kama haya yote yatakuwa magumu basi form hizo nazifutwe kabisa ili kukilinda chuo na ufisadi huu! Inatia aibu sana pale ambapo wasomi wanashindwa kuwasadia na kuwafanya wawe walarushwa wa kesho!
Yangu ni hayo tu. Lakini kumbuka hata ugawaji wa vyumba (accommodation) nao umezungukwa na rushwa isiyosemekana. Mulika na hilo pia. Ma warden huwa hawahusiki moja kwa moja. Wanachofanya huwatumia wanafunzi waliotangulia (continuing) kuuza vyumba. Hawa wanakuwa ni middle men ama kwa lugha nyepesi madalali wa vyumba. Hupata mgawo toka kwa ma warden. Mchezo huu ni mchafu zaidi. Yafanyie kazi.