Prof. Mukandala Maliza Rushwa hii UDSM

Prof. Mukandala Maliza Rushwa hii UDSM

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
1,272
Reaction score
1,120
Wanajamvi nawasalim sana!
Licha na kutingwa na majukumu yangu ya hapa na pale naomba nitumie muda huu kumuomba makamu mkuu wa chuo kikuu (mother of all universities) udsm kuzui rushwa hii. Prof. Wangu natambua anakabiliwa na majukumu ya kuhakikisha taaluma za vijana wetu zinatolewa kwa ufanisi mkubwa sana hivyo kukifanya chuo kubaki kwenye rank za juu kitaaluma. Majukumu haya hayapishani na yale ya kisiasa na kule synovate!

Mkono wangu naunyoosha pale dispensary ya chuo. Sote tumeona vijana wetu wakijiunga na chuo siku hizi chache toka vyuo mbalimbali. Kwa mlimani (sina hakika na kwingine) kuna utamaduni wakuanzisha miradi baada ya first year kujiunga. Miradi hii imekuwa ya kukusanya fedha toka kwa vijana hawa bila mpangalio. Kutokuwa na mpangilio na utaratibu wakueleka mdudu rushwa na ufisadi wa hali ya juu anazidi kuwatafuna watoto wetu.

Pamekuwa na tozo ya Tsh 5,000/- kwa kila mwanafunzi anayetaka kujaziwa fomu ya matibabu. Fomu hii imekuwa ni moja ya kigezo muhimu kuweza kufanikisha zoezi zima la admission kwa mwanafunzi. Well, binafsi sipingi uwepo wa form. Ninachokipinga hapa ni mchakato mzima wa ujazwaji wa form hizo unaoambatana na mikono mochafu ya rushwa. Nilifanikiwa kufika dispensary hapo siku za karibuni kuweza kuangalia zoezi hilo. Nilichogund ua na kuthibitishiwa na wahusika (wanafunzi) ni kwamba huwa wanalipa kiasi hicho cha 5000 bila hata yakufanyiwa vipimo!

Nasema sipingi pia ulipwaji wa fedha hizo. Ninachopinga hapa ni ujazwaji wa form hizo pasi na kufanyiwa vipimo husika. Je lengo hasa la form hizo ni lipi? Hasa ikizingatiwa vijana hao hawapimwi?! Zoezi hili hata sisi lilitukumba nakulipa pesa hizo enzi tunajiunga na chuo. Inakera sana Prof. Naomba ulivalie njuga na ikibidi fanya uchunguzi kubaini tuhuma hizi. Zoezi hili limekuwa likiwaandaa vijana wetu kuwa watoa na wapokea rushwa mapema kabla hawajaanza hata masomo. Na wamalizapo vyuo ndiyo wanafikia kutufikisha kwenye Richmond na mikataba ya kipuuzi ya gas inayoendelea sasa.

USHAURI:
Prof. Rwekaza Mukandala, form hizo zitotelewe na zijazwe bure na madaktari wa hapo chuo. Ikumbukwe kuwa si kila mtu ana uwezo wakulipa hiyo 5000. Tumia wataalamu na taaluma yako kubaini wale wote wanaohusika na mradi huu na wawajibishwe. Ama pawekwe utaratibu mahususi utakaothibisha mtu amapimwa na amelipia (endapo italazimu iwe hivyo). Kama haya yote yatakuwa magumu basi form hizo nazifutwe kabisa ili kukilinda chuo na ufisadi huu! Inatia aibu sana pale ambapo wasomi wanashindwa kuwasadia na kuwafanya wawe walarushwa wa kesho!

Yangu ni hayo tu. Lakini kumbuka hata ugawaji wa vyumba (accommodation) nao umezungukwa na rushwa isiyosemekana. Mulika na hilo pia. Ma warden huwa hawahusiki moja kwa moja. Wanachofanya huwatumia wanafunzi waliotangulia (continuing) kuuza vyumba. Hawa wanakuwa ni middle men ama kwa lugha nyepesi madalali wa vyumba. Hupata mgawo toka kwa ma warden. Mchezo huu ni mchafu zaidi. Yafanyie kazi.
 
hyo ni kweli mkuu umenena yaan mtu unatoa elfu 5 bila ya kupima sa ina maana gan?watu wanaulipia muhuri na elf 5 siyo ya kupimwa
 
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wahalifu.over
 
Ndugu yangu Goodluck, Prof. Mukandala sio kwamba hafahamu hiyo rushwa, yeye ana fungu lake kwenye hayo makusanyo, sasa ni kiongozi gani usiyejua mambo yanayoendelea ndani ya taasisi yako na kuyafumbia macho kama hupewi mgawo? Prof. kama hutaweza kupiga vita rushwa hii tutaingilia kati, fanya sasa.
 
Je hizo fedha zinazotolewa wanapewa risiti? Na kama risiti hazitolewi uongozi wa hospitali/zahanati watajuaje wametoa huduma ya kiasi gani? Kwa kuadai fedha kwa ajili ya muhuri bila kumpima mtu huo ni kudhalilisha taaluma yao na pia ni rushwa.
 
Poleni wote tuliokosa mkopo,mimi ni kiongozi wa lile kundi la watu thelathini na 32,tuliokutana na kamati ya maendeleo ya jamii ya Mwenyekiti Mh.Magreth Sitta kuomba na kuishinikiza serikali kutupatia ada ya chuo,tuliangaika sana wiki nne barabarani ila mwishowe ikatolewa bilion 3.1,huwezi amini na juhudi zote jina langu halpo kwa wategemewa wa mkopo,hivyo basi kwa moyo mpya nimeamua kuanzisha harakati nyingine ambayo itawashilikisha wakuu wa nchi hii hadi Mh.Rais,ninaimani sana bodi wanafanya mambo kinyume hawako kwa masilahi ya wanafunzi na umma wapo kwa masilahi yao,hivyo basi kwa yeyote anayejua kuwa suala la yeye kukosa mkopo kwake ni hujuma na hajalidhka na maamuzi ya bodi mfano kupewa sababu feki kama kumaliza shule miaka mitatu nyuma na sio kweli,kutuma fomu ya maombi bodi na yeye kuambiwa hajatuma na wakati una list ya EMS,kutukanwa na wafanyakazi wa bodi kwa aina yoyote ile tafadhali tuwasiliane kupitia 0712177649,tushrikiane kwa ili.HAKI INACHELEWESHWA ILA HAIDHULUMIWI.
 
Back
Top Bottom