MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Nimetazama taarifa ya Habari ya leo kwenye kituo kimoja cha television taarifa ya Mungai kuwa tatizo la kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne si kwa sababu ya migomo, ila ni kwa sababu walimu hawafundishi kwa masaa matano na robo kama inavyopasa, bali wanafundisha kwa masaa mawili tu, Hivyo alimaliza mzee huyu kuwa hakukuwahi kuwa na mgomo wa walimu hapa Tanzania, ilisema sehemu ya hotuba yake.
MY TAKE: Mungai hajui kuwa kuwa na akili si lazima usome hadi ngazi ya uprofesa, ni uwezo wa kuchambua mambo tu na kuyatolea tafsiri. Kama walimu hawafundishi kwa masaa matano na robo (sijui ni kwa siku, wiki au mwezi) kama inavyopasa badala yake wanafundisha kwa muda wa masaa mawili tu, huu sasa ni nini kama sio mgomo??? je hakuchemsha hapa?