Prof mungai: Hakukuwahi kuwa na mgomo wa walimu tanzania

Prof mungai: Hakukuwahi kuwa na mgomo wa walimu tanzania

MAKOLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
618
Reaction score
280
Nimetazama taarifa ya Habari ya leo kwenye kituo kimoja cha television taarifa ya Mungai kuwa tatizo la kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne si kwa sababu ya migomo, ila ni kwa sababu walimu hawafundishi kwa masaa matano na robo kama inavyopasa, bali wanafundisha kwa masaa mawili tu, Hivyo alimaliza mzee huyu kuwa hakukuwahi kuwa na mgomo wa walimu hapa Tanzania, ilisema sehemu ya hotuba yake.

MY TAKE: Mungai hajui kuwa kuwa na akili si lazima usome hadi ngazi ya uprofesa, ni uwezo wa kuchambua mambo tu na kuyatolea tafsiri. Kama walimu hawafundishi kwa masaa matano na robo (sijui ni kwa siku, wiki au mwezi) kama inavyopasa badala yake wanafundisha kwa muda wa masaa mawili tu, huu sasa ni nini kama sio mgomo??? je hakuchemsha hapa?
 
Mungai kawa profesa tangu lini acha kuonyesha ukilaza wako hapa
 
mungai yupi huyu? yule alieanzisha somo la physics with chemistry!
 
Mungai hana moral authority ya kulizungimzia suala la elimu kwa sasa kwani hata yeye ni mmjawapo wa kulaumiwa ktk kudumaza maendeleo ya elimu nchi hii, hakumbuki mitihani alivokuwa anavujisha mpaka makaratasi mengine wauza maandazi wanafungia wateja wao maandazi?, hakumbuki alivo ya baka masomo ya physics na chemistry na kuyafanya yawe somo moja? aache pombe!!!!!!!
 
Back
Top Bottom