Prof. Ndalichako, watazame hawa watoto wakiwa wanakwenda shuleni

Prof. Ndalichako, watazame hawa watoto wakiwa wanakwenda shuleni

Ni wapi hiyo? Madogo wanapata taabu ila wako vizuri, ni wapambanaji kinyama hao 😁😁
na nakuambia watoto wa namna hiyo usishangae kukuta zinachaji kuliko hawa wa kupelekwa na mataxi shuleni
 
kuna mambo kiufupi serikali inapata shida wananchi wake.

mimi nipo vijijini kwa sasa.hawa watu wa vijijini yeye akiona watu wameongeza maeneo hayo.analofanya ni kusogea zaidi maporini ambako si kitu rahisi kufikisha huduma.

vijiji vingi kukusanyika sehemu mmoja ni ngumu. utafikisha huduma ngapi kila kona.

watu wa vijiji yuko tayari kukaa unbali kilomita 4 na jirani mwenzake. ilimradi kujitenga.

na hii ndio kasoro baazi ya vijiji huduma kufika
 
Tz safari bado ni ndefu, hapo ni wenye moyo wanaenda shule bado walioamua kuolewa na kuwa wavuvi hatujawaona.
 
Dan
Ni shida tupu huko vijijini...wako wanafunzi wanaoliwa na mamba marneo mengine, pia wanyama wakali Kama fisi na chui...pia chatu....yaani vijijini maisha ni shida...lakini viongozi wachache wanaliona hili...Mungu mkubwa...

Hizi shule ni mpya au zilikuepo miaka mingi? Au ndio kama wale watoto wanaotoka pugu na gongolamboto kwenda kusoma bunge primary na Olympio?

Kuna wazazi wako radhi kumpeleka mtoto shule wanayoipenda wao bila kuangalia mtoto anapitia changamoto gani huko njiani.
 
Back
Top Bottom